Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia meshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu.
Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao lilitibuka.
Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano yangali yanaendelea.Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.
Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.
Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.
Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/02/140221_alshabaab_ikulu.shtml
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments