[Mabadiliko] TUJIKUMBUSHE YA CHADEMA MPYA NA RUZUKU.

Monday, February 10, 2014
Huyu anayejiita Chadema mpya kwa sasa hajapost kwa muda hapa jukwaani,
mtakumbuka kuwa aliweza kuishi kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua
japo kuna majina mengine bandia yalikuwa yanang'olewa kwa kasi ya
kimbunga! Huyu Chadema mpya kwenye nyaraka tofauti tofauti tulizokuwa
nazo naza mawasiliano binafsi anaoneka kuwa ni yule Mwalimu wa chuo
kikuu.

CHADEMA Mpya
<chademampya2014@gmail.com> Fri, Oct 18, 2013 at 2:26 PM
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Reply | Reply to all | Forward | Print | Delete | Show original

Tangu Zitto atoe agizo la vyama vya siasa kukaguliwa kwa niaba ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kumezuka malumbano mbalimbali
dhidi ya Zitto (Personal Attack) badala ya Kamati kwa ujumla toka kwa
watu mbalimbali lakini zaidi sana toka CHADEMA na CCM.

Kwa mtazamo wangu ndani ya CCM na CHADEMA wanaomshambulia Zitto
wanafanya makusudi na kwa malengo ya kisiasa. Wanataka watu waone
agizo lile ni la Zitto na sio la Kamati ya Bunge na kwamba Zitto ana
agenda binafsi jambo ambalo sio kweli na ni Propaganda tu.

Ndani ya CHADEMA kuna watu wanataka kumfitinisha Zitto na WanaCHADEMA
kwa malengo binafsi lakini hasa hasa ni ya Uchaguzi ndani ya Chama
chao. Wanataka WanaCHADEMA waamini kuwa Zitto anataka kuzuia ruzuku
ili wapate shida na washindwe kufanya kazi za Chama na wale wa Makao
Makuu wakose mishahara yao ya kila mwezi. Wanajua na wanaamini kwa
kufanya hivyo watu wao ndani ya Chama watamchukia Zitto na ukija
uchaguzi Zitto hatapata Uenyekiti (Maana anautaka na yuko very serious
wakati huu kuliko wakati mwingine wowote). Lakini Zitto alishasema
hadharani kuwa yeye hana wasiwasi na hesabu za CHADEMA maana ziko safi
anataka kuwabana CCM.

Ndani ya CCM kuna mitandao ya Urais ambayo kila uchao inahangaika
kuingiza fitina ndani ya CHADEMA ili viongozi wagombane Chama
kisambaratike ili wao wapite kwa urahisi. Wanajua hata kama
watapitishwa na CCM wakati CHADEMA ikiwa bado ni imara hawatafanikiwa
kuingia Ikulu. Inasemekana mitandao hiyo ya Urais ndani ya CCM ndio
ambayo pia imekuwa ikilipua mabomu kwenye mikutano ya CHADEMA kwa
kuloby Ma OCD na Ma RPC ili watu wafe kwenye mikutano ya CHADEMA watu
waiogope CHADEMA kabla ya 2015. Kwa hiyo Mitandao hii ya CCM
inachokifanya ni kuchochea fitina na Migogoro ndani ya CHADEMA kwa
kumgombanisha Zitto na Viongozi wenzake na WanaCHADEMA pia kwa njia ya
Propaganda ila kwa sababu CHADEMA nako Zitto ana maadui basi
wanaungana na hawa wa CCM kumshambulia Zitto. Zitto stand on Issues
and Truth Time will solve everything.

--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
Alternative: +255 (0) 784 24 67 64
Skype: Mohamedi.Mtoi
Twitter: @mohamedimtoi
Facebook: http://www.facebook.com/mouddymtoi
--

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments