[wanabidii] USHOGA NA USAGAJI NDANI YA TANZANIA

Sunday, January 19, 2014

Ni matumaini yetu kuwa wikiendi imeanza vizuri kwa wenzetu wote ulimwenguni popote walipo,sisi tunashukuru mpaka sasa hivi mambo yote yanaendelea kama yalivyopangwa hatuna budi kumshukuru mola wetu mlezi alietuumba sisi na alie umba mbingu na ardhi.

Kama kawaida yetu kuwa mara kwa mara tunakuwa tukiandika vitu mbali mbali katika kuboresha jamii yetu ya Kizanzibari kimawazo na kifikira na Tanzania kwa ujumla.

Kitu ambacho kimekuwa mawazoni mwetu kwa muda mrefu sana na tumekuwa tukikifikiria jinsi gani ya kukiandika bila ya kuanzisha mjadala wa matusi na maneno yasiyokuwa na maana na watu kutukanana,ila leo tumeamua kuvua nguo na kuingia kwenye maji ili tukoge,tunachotaka kukizungumzia leo ni UBARADHULI katika visiwa vyetu vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Ijapokuwa kuna watu kadhaa hususan katika nchi za nje Ulaya pamoja na Marekani jambo la ubaradhuli linakubalika hata katika viwango vya juu katika serikali,sisi tunazungumzia kwa mujibu wa imani yetu ya dini ya Kiislamu,kwamba jambo hili katika uislamu halikubaliki,na sio katika dini ya Kiislamu tu hata katika Ukristo,Uhindi,Uyahudi pamoja na Bhudda hakuna hata moja kati ya dini hizi zinazokubali ubaradhuli,sio katika Qur-an wala sio katika Biblia zote zinapinga vitendo vya Ubaradhuli.

Kwanza ikubalike kuwa Zanzibar vitendo vya Ubaradhuli vya kuingiliana wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake na kufanya mapenzi vimezidi,vimezidi kiasi ambacho watu tumeanza kuona mambo haya ni ya kawaida miongoni mwa watoto wetu na jamaa zetu,kuna wanaofanya haya kwa njia ya kujificha ya siri na kuna wale wanaofanya kwa dhahiri,haijalishi kama unafanya kwa siri au kwa dhahiri kama unafanya ndio unafanya tu,kumbuka kuwa sio sisi tunaohukumu ila anaehukumu ni yule ambae aliyekuumba.

Picha tulioiweka hapo juu hatukuiweka hapo kwa ajili ya uchochezi au kwa ajili ya kuwaadhirisha watu fulani,na kwa kweli hatuwezi kuita ni muadhara au kuadhirishana kwa sababu wao wenyewe wanaona ufahari,imefika wakati kama mnavyoona hapo kwenye picha kuwa wanaume wanavaa mabui bui na kanzu pamoja na kuchana misuko na mapodari kama wanawake,yote tunayaona lakini je wangapi tunakemeya vitendo hivi.

Kuna habari tofauti vipi watu wanakuja kuwa mabaradhuli,kwa ukweli sisi hatuna uhakika kivipi mtu anakuwa baradhuli ila jambo moja ambalo tunalifahamu kuwa mtu hawezi kuwa baradhuli bila ya kuwa na basha ndio maana kwa mujibu wa lugha ya kiswahili ukisema khanithi siku zote tunajua ni yule ambae anaependelea kuwa mwanamke na yule anaemuinamisha tunamwita basha,lakini ukweli wa mambo wote ni makhanithi,anayeingiliwa anakhanithiwa na anaemuingilia mwenziwe ni khanithi.

Kuna watoto humu ambao wanaharibiwa tokea wadogo bila ya wazazi wao kujua,na je unajuwa kwanini wazazi wao hawajui ?hususan mababa wa watoto hao,ni kwa sababu baba aidha kaendekeza kufuata wanawake nje ya ndoa,kwenda kucheza karata na bao maskani,au kwenda kuzungumza siasa zisizokuwa na mbele wala nyuma,bila ya kujali kujua mwanawe kafanya nini wala kujua shule kasoma nini.

Mtoto umleavyo ndivyo hivyo hivyo atakavyokuwa ikiwa umemuweka mwanao kama rafiki yako na kutaka kujua kila analolifanya na kuzungumza nae na kumuelewesha umuhimu wa maisha lipi zuri lipi baya,ni hakika kabisa akija kulawitiwa atakwambia,au chochote kibaya kikimtokezea atakwambia,la ikiwa huna habari nae,huna hata siku moja ulokaa nae chini ukazungumza nae kama kuna tatizo gani,huna siku ulotoka nae ukaenda nae kwenye mpira au kumfundisha kwenda kuogelea pwani basi ni uhakika kuwa mtoto huyo atakuwa hana habari kama wewe,mara nyingi vitendo kama hivi vinajionesha pale vikianza tu,na kama wewe mzazi kweli unamjua na kumweka mwanao karibu basi utagundua,lakini wengi wetu hatugundui haya kwa sababu dunia ya nje tumeiweka mbali,mkeo akikwambia leo mtoto wetu kachelewa kurudi kubwa unalolifanya ni kuchukua mkwaju au mkanda na kuanza kumcharaza,huna sumile hujui kuuliza alikuwa wapi au nini kimetokea,na kama kweli kupiga ingekuwa kuna muweka mtoto sawa mbona manunda yamejaa na mabaradhuli wanazidi kuongezeka?

KWENU NYINYI WANAWAKE.

Ndani ya mtandao huu wa usobuku kuna picha chungu nzima pamoja na comments ambazo wanawake dada zetu mama zetu na ndugu zetu mmepiga nao hawa mabaradhuli na kuwapa kila sapoti ili waendelee wanayoyafanya,mnawatunza kwenye mataarabu wakiweka picha mnaweka komenti za kuwahamasisha ili waendelee kufanya wanayoyafanya,hatuna haja ya kutaja majina wenyewe mnajijua,lakini suala la kujiuliza je ingelikuwa mwanao ndio baradhuli kaweka picha kama hiyo ungeliwacha koment ya kumhamasisha aendelee na ubaradhuli au ungejitoa kwenye mtandao wa usobuku ili usione ya mwanao anayoyafanya?Bila ya shaka usingewacha koment kwa sababu kijiso chako kingekuwa kidogo na mwanao angekuwa anakula roho kila siku,sasa kama kwako wewe sio mazuri kwanini yawe mazuri kwa mwenzio?
Rudi kwa Mola wako mlezi kama unajumuika nao hawa wacha mara moja,haifai,sio vizuri wala sio utu,jiengue na uwe mbali nao kwa njia yoyote na ikiwezekana zungumza nao na uwaelimishe kuwa wanayoyafanya sio na si mazuri.

KWA MABASHA.

Nyinyi ndio chimbuko la hawa mabaradhuli,nyinyi ndio mahasidi na washenzi wenye husda kila pahali mko tayari kumharibu kila kijana mnaemuona,mnapenda wanaume na watoto wa wenzenu kuliko wanawake mliohalalishiwa na Mola wetu mlezi,mmekuwa hamna haya wala hamjui vibaya,kimeme kimekutokeni,nyuso zenu zimebadilika mkimuona mtoto mzuri wa kiume mnamahanika hamjui mnalolifanya uhasidi na hasada zilizochanganyika na fitna na choyo ziko kwenye nyuso zenu,mnasawajika,mnasahau kila kitu,mnasahau dini,utamaduni,mnasahau,silka pamoja na thakafa zetu,tunakwambieni nyie msokuwa na haya muwache kuharibu watoto wa watu,rudini kwa Mola wenu mlezi mtubie.

KWENU NYINYI MABARADHULI.

Ijapokuwa unachokifanya unakiona ni kizuri lakini moyoni mwako unajuwa kuwa unachokifanya sio kizuri na tuna hakika unasema kuwa kuna siku nitatubiya lakini kwa vile hatuna miadi na Mola wetu mlezi siku gani utaumwa na kufariki kabla hujatubia ndio maana bado mnaendelea kufanya haya,na wangapi wanakufa kabla ya kutubia,wangapi ushawahi kuwaona wametoka nyumbani kwao wakiwa wazima kuanguka na kurudi maiti,au kugongwa na gari kufa hapo hapo,haifai jamani tukisahu kiburi na tusiyape matamanio yetu yakawa uongozi wetu Mola wetu mlezi ni mwingi wa msamaha,tubia wacha haya rudi kwa Mola wako na uombe msamaha,la ikiwa mtaamuwa kuendelea kufanya mnayoyataka tunaomba mfanyane wenyewe kwa wenyewe,bila ya kuwalaghai watoto wetu na kuwapa zawadi tunajuwa kuwa baadhi yenu mnakaa nje ya nchi,mnaona zawadi zenu ndio njia moja wapo ya kupata mnalolitaka,lakini kumbuka kuwa kuna siku watu watakusahau na ardhi ndio yatakuwa makalio yako pamoja na malazi yako,kwa hiyo kama kiburi chako ndio unaona kinga yako kubwa basi jua kuwa kiburi chako kamwe hakitamfikia firauni.
Na ujue kuwa kama wewe ni baradhuli wa kiume unaejifanya mwanamke wewe utabakia kuwa mwanamme tu,halikadhalika wewe mwanamke unaejifanya mwanamme wewe ni mwanamke tu.

KWA VIONGOZI WETU.

Tunakumbuka hapa mwishoni mwa miaka ya tisini kuna baradhuli mmoja kutoka Mombasa alipewa masaa ishirini na nne aondoke nchini baada ya kufunga ndoa na mwanamme mwengine Zanzibar,huo ulikuwa ni wakati wa Muheshimiwa Salmini Amour Juma,lakini leo hii wanaume ndio wanavaa mpaka mabui bui hadharani na hakuna kinachotokea,watu hata hatutetereki,na serikali inayoongozwa na Maraisi watatu wote Waislamu,Muheshimiwa Sheni,Muheshimiwa Balodi Iddi pamoja na Muheshimiwa Hamad,uwaone mstari wa mbele ikifika Ijumaa nyuso zimesimama vizuri kwa Sijda zao lakini kitendo kama hiki kukikemea midomo yao imefungwa nanga mizito,wanaogopa wamekuwa kama shetani aloona Mcha Mungu,hawawezi kusema hata kwii.

Kumbukeni waheshimiwa kuwa iko siku kila mchunga ataulizwa kwa kile anachokichunga kwa hiyo sisi na nyinyi na kila mmoja tukaeni mkao wa kula ikiwa mabaradhuli wamekaa mkao wa kuliwa.
Inapokuja adhabu ya Allah haichagui,na tutalaumu Muungano na kila jambo lakini vitendo vyetu wananchi ndio vitakavyo bashiria maendeleo ya nchi yetu,sote tunajua machafu yakizidi neema inaondoka,na sasa hivi haya yote tunayaona,mabalaa ya bahari,joto limezidi kupindukia,uchawi kila mtu anaroga waganga kila kona,wizi,madawa ya kulevya,watu waongo,utapeli,mabasha na mabaradhuli kila pahali,umalaya,walimu kulala na wanafunzi haya yote ni uchafu na kama tunavyojua tukiendelea kufanya machafu basi na viongozi wetu watakuwa wachafu na wana ukosefu wa uadilifu,kwa hiyo ijapokuwa Muungano wetu una matatizo yanataka yarekebishwe ila matatizo yote yanaanza kwetu wenyewe sisi wananchi kwa mambo ambayo tunayafanya.

Hali hii haiko Zanzibar tu kwa sasa hivi imeene kila pembe kutoka Dar-es-Salaam,Mtwara,Arusha na kila pembe katika Afrika mashariki.

Tuwacheni mambo haya na kama wewe mwanamme unaejiita Basha unaependa wanaume kaowe umuweke mke ndani,na mababa mkae na watoto wenu muwaelimishe samaki mkunje angali mbichi.

Tunaomba maoni yenu na kwa ihsani zenu toa maoni yenye akili matusi,kejeli dharau ya aina yoyote kwa mwenzio tutakutoa.

Picha tuliyoiweka hapo sio mpya takribani kila mtu kishaiona tulichofanya sisi ni kuichukua na nyinyi mujionee hali khalisi,kwa hio kusikuweko na mjadala kwamba kwanini tumeweka picha,lengo ni kuzungumza kwa uthibitisho na huo ndio uthibitisho wetu.

AHSANTENI

VOICE OF ZANZIBAR

TAFADHALI SHARE NA WENZAKO

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments