[wanabidii] Tuwekeze Zaidi katika Lugha za Asili

Sunday, January 19, 2014
Tuwekeze Zaidi katika Ufundishaji wa Lugha za Asili 

Ndugu zangu ,

Wiki hii tumekuwa na Usaili wa watu kadhaa ili kupata watu wa kuweza kufanya shuguli mbalimbali katika jamii , katika usaili huu kuna mambo kadhaa yamenistajabisha na kunionyesha kwamba kama taifa tunatakiwa kufanya mabadiliko kwenye Lugha .

Usaili ulikuwa mgumu sana kuendesha kwa lugha ya kiingereza kutokana na vijana wenyewe kutokuwa na uwezo wa kumudu vizuri lugha ya kiingereza kama vile inavyotakiwa .

Basi iliamuliwa mtu achague lugha anayotaka kufanyiwa Interview , wengi walichagua Kiswahili , baadhi walitaka mchanganyiko kati ya Kiswahili na kiingereza na wengine walichagua lugha zao za asili .

Hapa kwenye lugha ya Asili haswa kwenye kisukuma watu wengi wameonyesha kuijua lugha hii na kuwa na umahiri wakujieleza vizuri kwa kutumia kisukuma kuliko Kiswahili na kiingereza .

Hii imenikumbusha Pale mawaziri wa kichina wanavyokuja nchini na wakalimani wao kwa kuwa hawajui kiingereza au wanababaisha , sisi pia tunaweza kuwa na wakalimani wetu wa kisukuma na Kiswahili au lugha nyingine na kujadiliana na wengine hata kwenye mikutano ya umoja wa mataifa .

Nadhani ni wakati sasa kwa serikali kupitia wadau wa elimu kufikiria zaidi kuboresha lugha zetu za asili kwenye uwanja wa elimu ili watu waweze kuzitumia vizuri zaidi huko mbeleni .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments