[wanabidii] Angalizo na Salamu za Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa Wahariri

Tuesday, December 31, 2013
MEDIA ADVISORY 

KWA WAHARIRI WOTE


Wakubwa Wahariri

Naungana nayi katika kuumaliza vizuri Mwaka 2013. Aidha, nachukua nafasi hii kuwatakia Heri nyingi za Mwaka 2014. Uwe ni mwaka wa Baraka na Mafanikio kwetu sote.

Napenda pia kuwapongezeni nyote kwa detailed reporting ya shughuli ya jana ya Kukabidhiwa kwa Ripoti (which includes Rasimu ya Katiba)  ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na Mheshimiwa Rais Ali M. Shein. Ni kazi nzuri – well done!

Jambo moja tu la msingi ambalo Mheshimiwa Rais Kikwete alilisisitiza jana ni kwamba there already appears some sections
of the Press ambazo tayari zimeanza kupotosha shughuli nzima ya jana kwa kuielezea Ripoti ya jana kuwa ni Katiba Mpya.

Naamini kuwa kila mmoja wetu anajua kuwa Ripoti ya Tume ambayo inashirikisha Rasimu ya Katiba,  siyo Katiba Mpya. Mchakato wa kupata Katiba Mpya ndio kwanza umeingia katika hatua nyingine, hatua muhimu sana. Ripoti ya Tume, ikiwa ni pamoja na Rasimu ya Katiba, lazima viende sasa kujadiliwa katika Bunge la Katiba.

Na hata baada ya kujadiliwa na Bunge la Katiba na Wabunge wa Bunge hilo kufikia maamuzi, ni kwamba maamuzi hayo lazima yaende kwa wananchi kwa ajili ya Kura ya Maoni – Referendum. Ni sisi wananchi ambao tutaamua, Kwa sasa tunaendelea kutumia Katiba ya sasa na hakuna Katiba Mpya.

Natumai kuwa tuzingatie ukweli huu wakati tunaendelea kuandika na kutangaza habari za jambo hilo kubwa na la kihistoria katika nchi yetu.

Once again – A Happy and Prosperous New Year to us all.

SALVA RWEYEMAMU  
MKURUGENZI WA MAWASILIANO
IKULU, 

DAR ES SALAAM.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments