NAOMBA NIANZE KWA SWALI KABLA YA CHOCHOTE;
Unapopatwa ajali mbaya na unahitaji watu wakusaidie ili kuokoa maisha yako lakini unawatu wako bize kupiga picha za tukio na wewe kukupiga picha ili warushe kwenye mitandao ya kijamii huku ukiendelea kuumia , utachukuliaje suala hilo ?
Watanzania sasa tumekosa utu kabisa yaani inasikitisha kuona tunapofika sehemu ya ajali tunashindwa kutumia muda wetu na nafasi hiyo kuwasaidia waliopata ajali na badala yake tunajikita zaidi kwenye upigaji wa picha za kurusha kwenye mitandao ya kijamii, huu ni ujinga mkubwa sana ambao watanzania tumeupata kwa sasa, hii inanionesha kuwa baada ya kumaliza ujinga fulani kwa mwanadamu huja ujinga mpya ambao pia utahitaji kuondolewa kwa nguvu kubwa.
Watanzania wenzangu akina mama na wanaume tunaomba sana turejee maadili na tamaduni zetu za kitanzania, utamaduni tunaouendekeza utamaliza ndugu zetu na itakuwa chukizo na laana mbele za Mwenyezi Mungu, watu inapofika sehemu wanakufa kwa uzembe wa watoa msaada si sawa kabisa na huyu afanyae haya naomba ahukumiwe kama muuaji maana huenda juhudi zake zingeweza kuponya maisha ya watanzania wenzetu.
Mambo haya hupelekea kuwa na watoto yatima na ombaomba wengi kwa uzembe wetu wananchi, tunapoteza nguvu kazi kubwa ya taifa wataalamu wa mambo ya human resource watakuwa wanajua vyema naongelea nini hasa, hatukatai kupiga picha ! piga lakini ikiwa tayari watu wale wameshapata msaada wako kama kwenye gari mshawatoa na huduma zingine za msingi zimeshatolewa, utajisikiaje mzazi wako, mdogo wako, dada au kaka yako ukishuhudia akikata roho kwa kukosa watu wakukusaidia kumtoa sehemu ya ajari na kumpa huuduma huku ukiona watu wote wanapiga picha tu na kuweka kwenye mitandao ya kijamii ??
Uhai wa ndugu zetu ni zaidi ya sifa tunazokimbilia kupost mitandaoni, hivyo vyema tukathamini maisha yao maana human is our fundamental resource.
Baada ya kutolea ujinga fulani mwanadamu hupatwa na ujinga mwingine maana ujinga hauna kikomo ila ulewa hufika kikomo, hivyo tuzidi kuelishana siku hadi siku, kizazi mpaka kizazi.
Kwa hili tunayo safari ndefu ya kujirekebisha ndugu zangu, naomba kuwakilisha hoja mezani kwenu mnisaidie kuelimisha jamii
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments