THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Clinton: Watanzania wana kila sababu kujivunia Serikali yao
Rais wa 42 wa Marekani, Mheshimiwa Bill Clinton amesema kuwa Watanzania wanayo kila sababu ya kujivua ukweli kwamba wanayo Serikali ambayo inaongoza katika kila ubunifu wa kuboresha kila lililo jema kwa ajili ya wananchi kwa nia ya kujaribu kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi.
Aidha, Rais Clinton amesema kuwa kama taasisi yake ya Clinton Fondation kupitia Mradi wake wa maendeleo wa Clinton Development Initiative (CDI) itashindwa kuhakikisha kuwa mradi wake wa kilimo ambao inauanzisha nchini unakuwa endelevu, basi Clinton Foundation yenyewe itakuwa imeshindwa.
Rais Clinton ameyasema hayo leo, Jumamosi, Agosti 3, 2013, Ikulu, Dar Es Salaam, wakati alipozungumza kwenye sherehe ya kutiwa saini kwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Clinton Foundation, ambako taasisi hiyo itasaidia maendeleo ya kilimo na wakulima wadogo wadogo kwa kuboresha kilimo chao, kiwango chao cha mazao, ubora wa mazao yenyewe na hivyo kuinua kipato chao.
Mara baada ya Rais Clinton na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wameshuhudia kutiwa kwa
saini kwa Makubaliano hayo, Rais Clinton aliwaambia waliohudhuria sherehe hiyo wakiwamo wakulima 10 kutoka mkoa wa Iringa na waandishi wa habari:
"Makubaliano haya ni mfano mwingine wa jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya watu wake. Kwa hakika, watu wa nchi hii lazima watembee kifua wazi na wanayo kila sababu ya kujivua ukweli kuwa Serikali yao inaongoza katika kila ubunifu wa kuboresha kila lililo jema kwa ajili ya wananchi kwa nia ya kuboresha maisha yao."
Ameongeza Rais Clinton: "Wakati nikizungumza na wakulima hawa, liko jambo limesemwa, kwamba zipo taasisi nyingi zinazokuja Tanzania zinaanzisha miradi kwa mbwembwe lakini miradi hiyo inakosa uendelevu na hivyo kufa baada ya taasisi hizo kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini. Hili halitatokea kwa mradi huu wa kilimo kwa sababu kama mradi huu utakosa uendelevu basi sote tutakuwa tumeshindwa".
Mapema marais hao wawili wamekutana na kuzungumza na wakulima wadogo wadogo 10 kutoka Mkoa wa Iringa, ambako CDI imeanza shughuli zake katika kilimo na ambako Makubaliano yaliyotiwa saini leo yataelekeza nguvu zake.
Amesema kuwa chini ya mradi huo litaanzishwa shamba la mfano (anchor farm) kwa ajili ya wakulima kuona mbinu mpya na bora za kilimo, kutoa mafunzo na kushiriki uzalishaji. Amesema kuwa mashamba ya namna hiyo yamefanikiwa sana katika nchi nyingine za Afrika ambako CDIinaendesha shughuli zake ikiwamo Malawi.
"Katika Malawi tulianza na shamba moja na sasa kuna mashamba ya mfano 21 ambayo yamekuza kipato cha wakulima mara tano na kuongeza uzalishaji mara mbili unusu."
Akizungumza kwenye sherehe hizo, Rais Kikwete ameisifu sana Taasisi ya Clinton Fondation kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania katika miaka 10 ambayo taasisi hiyo imekuwepo Tanzania na hasa katika nyanja za afya na sasa kilimo.
Mheshimiwa Clinton ambaye amekaa Ikulu kwa kiasi cha saa tatu pia amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Kikwete kuhusu masuala mbali mbali. Rais Clinton ambaye yuko katika ziara ya siku mbili nchini ataondoka kesho, Jumapili, Agosti 4, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Agosti, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments