maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Chama hicho Wilaya ya Musoma cha
kuwavua Uanachama madiwani wawili wa viti maalum Habiba Ally Zeddy na
Mariam Daudi Chacha na hivyo kupoteza sifa ya kuwa madiwani kwa mujibu
wa Katiba ya Chama hicho.
Katika barua iliyotumwa na Afisa Sheria wa Chama hicho Ester Daffi
yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/10/101 ya tarehe 22/2/2013 kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Willbord Slaa ilisema kama kuna
utovu wa nidhamu kwa wahusika ilitakiwa kuzingatia masharti ya Katiba
na Kanuni hasa kanuni ya Uendeshaji kazi za Chama ibara ya 6.5.2
pamoja na Kanuni ya 8.0 (a) na (b) ya nidhamu kwa madiwani.
Katika barua hiyo ilidai suala hilo lilitakiwa kutolewa taarifa Makao
Makuu kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye Kamati Kuu kwa ajili ya maamuzi
kwa kuwa mamlaka ya kuwavua Uanachama yanapaswa kuzingatia kanuni
tajwa ya katiba ya Chama hicho.
Alisema Makao Makuu ya Chama hicho imepinga maamuzi hayo kutokana na
madiwani hao kukata rufaa kupinga maamuzi hayo katika barua yao ya
rufaa iliyotumwa kwa njia ya nukushi tarehe 21/2/2013 na kuipitia kwa
kina na kisha kutoa maamuzi hayo kwa mujibu wa katiba.
Ilidaiwa katika barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa kwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma ilisema kamati ya Utendaji ya Chadema
Wilaya ya Musoma haikuzingatia barua kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa
Chama hicho ya tarehe 16/2/2013 yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/
101.
Katika barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha Habari (MGOGORO NDANI YA
HALIMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA) ilidai tarehe 15/2/2013 Mkao Makuu
ilipokea taarifa kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex
Kisurura kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya ya Halimashauri hiyo
ukihusisha baadhi ya Viongozi wa Chama wa Jimbo.
Katika barua hiyo ilidai Halimashauri ya Manispaa ya Musoma inaongozwa
na (CHADEMA) na kwa mujibu wa kanuni ibara ya 3.1 (a) (c) (g) na (i)
ya kanuni za kusimamia Shughuli,Mwenendo na Maadili ya Halimashauri
zilizo chini ya Chadema,Ofisi ya Katibu Mkuu kwa azimio la Kamati Kuu
ndiyo msimamizi wa shughuli za Halimashauri za Chadema Nchini.
Barua hiyo ilida Agenda kuhusu mgogoro ndani ya Halimashauri au
kutofautiana kwa Meya na madiwani na au Uongozi wa Chama isijadiliwe
mpaka mchakato wa ndani ya Chama utakapokamilika au kwa maelezo kutoka
Makao Makuu na pindi itakapokwenda kinyume hatua za kinidhamu kwa
mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama zitachukuliwa
dhidi ya wote watakaokiuka maelezo yaliyotolewa.
Akizungumza na blog hii mara baada ya kupokea barua ya majibu ya rufaa
kutoka Mkao Makuu ya Chadema,Diwani Habiba Ally Zeddy alisema licha
kushinda rufaa yao ya kuvuliwa Uanachama Makao Makuu inapaswa
kuangalia kwa karibu mwenendo wa Chama hicho Wilaya ya Musoma.
Alisema maamuzi ya kuvuliwa Uanachama waliyofanya Kamati ya Utendaji
na kutangazwa katika Vyombo vya Habari ni kama wamezalilishwa kwani
hadi sasa licha kutolewa maamuzi ya kuvuliwa hakuna barua yoyote
waliyopewa kuhusu kuvuliwa Uanachama na kukosa sifa ya kuwa madiwani.
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments