[wanabidii] JESHI LA POLISI LIMEJIWEKA NJIA PANDA?

Thursday, February 21, 2013

Jeshi la Polisi nchini, limejiweka njia panda, kufuatia taarifa yake kwa vyombo vya habari kukanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania toleo namba 7235 la Alhamisi 21.02.2013, yenye kichwa cha habri 'WATUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRE WAKAMATWA KENYA". Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kuwa habari hiyo ni ya Uongo.

 

Maswali ya Msingi. [Habari zote zinahusu  habari isiyo ya kweli dhidi ya polisi]

 

  1. Je Mwandishi wa habari hiyo wa Mtanzania atatafutwa na kupekuliwa chumba kama yule wa Tanzania Daima aliyeandika habari na baadaye kuomba radhi?

 

  1. Je Mhariri wa Mtanzania na Mwandishi wake watahojiwa kwa masaa zaidi ya sita, na kutolewa kwa dhamana Kama walivyohojiwa Mhariri na Mwandishi wa Tanzania Daima?

 

  1. Je Mhariri Mtendaji wa Mtanzania, na Mmiliki wa Gazeti hilo, na Mchapishaji watatafutwa kama wanavyotafutwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Mmiliki wa Gazeti na Mchapishaji ili wasaidie Polisi?

 

 

  1. Je Mtanzania litatishiwa kufungwa na Rais kama si huyu basi ni ajaye?

 

  1. Je Taaluma ya Mmiliki wa Gazeti la Mtanzania (Mfanyabiashara) itahojiwa kwanini anamiliki gazeti, kama walivyohoji Mmiliki wa Tanzania Daima kuwa Daktari lakini anamiliki gazeti?.

 

 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments