[wanabidii] Hamad Rashid abwagwa kortini

Wednesday, November 28, 2012
Kutoka uso wa kitabu wa Julius Mtatiro..
Julius Mtatiro

36 minutes ago via mobile


TUMESHINDA KESI YA AWALI AMBAYO MHE. HAMAD RASHID NA WENZIE WALIKISHTAKI CHAMA.

Hukumu imemalizika muda so mrefu hapa mahakama kuu.

Hoja zote za akina Hamad Rashid zimetupiliwa mbali.

Mahakama imejiridhisha kwamba, amri ya mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR na wenzake wanne haikufikishwa kwa chama kwa hivyo kikao husika kilikuwa halali.

Hii ina maana kw...amba OMBI la Hamad Rashid na mawakili wake kuwa WAJUMBE WOTE WA BARAZA KUU la CUF wafungwe jela kwa kukiuka amri ya mahakama limetupiliwa mbali.

Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013 ambapo mawakili wa chama watapangiwa tarehe YA kuleta hoja za kutaka kesi ya msingi ifutwe kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na walifukuzwa kihalali na kwa kuzingatia katiba ya chama.

Chama chetu kimefurahishwa na uamuzi huu kwani unaonesha namna ambavyo hatukukurupuka.

Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki.

My Take
Nini hatma ya Hamad Rashid kisiasa maana ni wazi upepo si mzuri kwake? Je ni wakati sasa wa CDM kufikiria kumpa nafasi Mh. Rashid ili kuendelea kujijenga visiwani Zanzibar baada ya kuwa na makada wa aina ya Profesa Safari? Ni wazi mchango wa Hamad Rashid katika kuleta mageuzi nchini si wa kubeza. Aliweza kuiongoza kwa ushupavu kambi ya upinzani bungeni 2005-2010 na ikaleta matunda mazuri. Pamoja na kuhusishwa na ADC (hakuna ushahidi) anaweza kupewa nafasi CDM? Tujadili hoja, bila matusi maana siku hizi jamvi limekuwa likichafuliwa mara kwa mara.
 Source http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/360415-hamad-rashid-abwagwa-kortini.html

Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 

Share this :

Related Posts

0 Comments