[wanabidii] Neno Fupi La Usiki: Ng'ombe Kipofu Na Aliyevunjika Mguu...

Tuesday, November 20, 2012
NDUGU zangu ,

Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Kwamba ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu. Wote watakufa njaa.

Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng'ombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako, na hata mahala pako pa kazi.

Tumekuwa jamii ya ovyo ovyo. Tunafanya mambo ya ovyo ovyo. Ni kutoka ngazi ya familia hadi ngazi ya kitaifa.

Tubadilike. Na hilo Ni Neno Fupi La Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments