[wanabidii] Kauli Ya JK Kuhusu Kifo Cha Daudi Mwangosi - Mwanzo

Tuesday, October 02, 2012

RAIS Jakaya Kikwete amezungumzia mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10, Daudi Mwangosi na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika suala hilo.

Akizungumza katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, Rais Kikwete alisema mauaji hayo ni ya kusikitisha na kuongeza; "Jambo la msingi ninalotaka kusisitiza ni polisi na kutendewa haki. Asiwajibishwe asiye husika."

Mbali na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika mauaji hayo, aliliagiza Jeshi la Polisi, pale panapotokea malumbano kati yake  na wafuasi wa kikundi cha kijamii au vyama vya siasa au wananchi, lazima wahakikishe hawatumii nguvu kupita kiasi, "Polisi lazima wahakikishe kuwa hawatumii nguvu kupita kiasi. Wao wenyewe wanatambua vyema maana yake.  Wanapofanya kinyume chake na ikathibitika hivyo nao pia huchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Haipendezi mbele ya macho na mioyo ya askari wetu lakini lisilobudi, hutendwa," alisema Rais Kikwete.


http://wotepamoja.com/archives/7909#.UGswhmEO3JQ.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments