[wanabidii] Deo Filikunjombe CHADEMA VS PIndi Chana CCM LUDEWA 2015

Tuesday, October 02, 2012
Juzi nilipita Ludewa nikakutana na wapiga kura wa Filikunjombe huyu
jamaa anapendwa sana. Tena ikumbukwe huko ndiko nyumbani kwa
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM Marehemu Kolimba. Kuna minong'ono
kuwa inawezekana kabisa Deo Filikunnjombe hawezi kurudishwa tena
kugombea kwa tiketi ya CCM mwaka 2015.

Huku kukiwa na majina kama ya Pindi Chana kuweza kurudishwa na CCM
kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimboni humo.

Sasa nikawauliza wadau hao kuwa inakuwaje sasa kwa Deo
Filikunjombe wakasema atakwenda CHADEMA na hakuna wasiwasi sisi
tutampigia kura bila shaka."Unajua hapa tulikuwa na shule zetu
za kata sasa zilikuwa zinajikongoja kumalizika kwani tulipewa
jukumu la kulenga mawe yakawa tatizo lakini kametusaidia sana
haka kakijana ketu sasa ni raha tu watoto wanasoma bwana."
anasema ndugu huyo.

Mbunge wetu anafikiria nje ya boksi hafikirini kwa kufungwa
ndani ya boksi ngoja tuombe uhai tu aliongeza mdau huyo.

Kwa kawaida eneo hili lina makabila ya Wakisi,Wapangwa , wamatengo
na wengineo ambao kwa desturi ni watu wapole na wanaheshimu sana
mamlaka. Kweni Katika safari yangu waliweza kutembea umbali mrefu
kuja kuhudhuiria mkutano ulionipeleka eneo hilo.

Sasa Deo Filikunjombe akigombea kwa CHADEMA na Pindi Chana kwa CCM
2015 hali itakuwaje Ludewa ?


Wasalaam Adeladius Makwega

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments