Hi All,
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi, amesema serikali ya Zanzibar imeshajitosheleza katika mfumo
wa serikali yake na haina haja ya kuwa na serikali ya Mkataba kwani kufanya hivyo ni sawa na kutaka kuvunjika kwa Muungano wa Tanzania.
Balozi Seif, alisema muundo wa serikali ya Zanzibar tayari umetoa fursa ya kuwa na vyombo muhimu vya juu ambavyo vimeweza kuunda serikali
na hakuna haja ya kutaka kuwapo kwa serikali ya Mkataba ambayo ni sawa na kuuvunja Muungano. Akifafanua kauli hiyo Balozi Seif alisema mfumo
wa serikali ya Zanzibar ndani ya Katiba umeruhusu kuwa na Katiba yake, Baraza la Wawakilishi, Muhuri, Bendera, Mawaziri, Wawakilishi na Wabunge
jambo ambalo tayari mfumo huo umejitosheleza.
0 Comments