Mwalimu Nyerere inasemekana alishindwa kuhakikisha chaguo lake linapita na badala yake Ndugu Ali Hasan Mwinyi akaichukua nafasi hiyo. Inasemekana chaguo la Mwalimu alikuwa Ndugu Salim Ahmed Salim.
Ndugu Ali Hasan Mwinyi angalau huyo tunafahamu hakuwa na chaguo. Ushawishi wake uliporomoka sana na karibu Mwalimu Nyerere alikuwa strongman. Hotuba zake zinazotoka kila mara kwenye luninga zinajieleza. Mwalimu Nyerere alifanikiwa kumpigia chepuo Ndugu Mkapa kwa hiyo Mwinyi hakufanikiwa kumpachika chaguo lake.
Wakati wa Benjamin Mkapa kung'atuka ilionekana alikuwa na chaguo lake japo kwa umahili wake haikuwa rais kumjua. Lakini kuna dalili kuwa Jakaya Kikwete hakuwa chaguo lake. Wakati wa mkutano mkuu wa CCM kuteua mgombea Mkapa alitoa hotuba iliyoashilia anammaanisha JK, lakini bado hakuwa chaguo lake.
Ndugu JK ameng'atuka. Alijitahidi kwa uwazi tena bila kificho kutaka kurithiwa na chaguo lake. Sitakuwa nimekosea nikiongeza kuwa kwa matamshi ya wanafamilia chaguo hilo halikuwa la JK peke yake bali lilikuwa la familia yake. Pamoja na makeke yote hayo mwisho wake JK hakurithiwa na chaguo lake. Kuna hisia kuwa ni Mkapa aliyefanikiwa kushawishi chaguo. Kama kuna ukweli ndani yake basi Magufuli alipita kwa uwezo wake na ushawishi wa Mkapa.
Dr. Magufuli ndiyo anaaza. Ana myaka minne iliyosalia lakini aweza kuendelea mpaka myaka kumi.
Dr Magufuli anaonyesha anaweza kurithiwa na chaguo lako kwa sababu kadhaa, zikiwamo zifuatazo:
1) Mtangulizi wake (JK) kama ilivyokuwa kwa Mwinyi haonekani kuwa anaweza kuwa na ushawishi mkubwa kuliko Magufuli wakati ukifika. Badala yake Magufuli anaweza kuwa na ushawishi mkubwa kiasi cha watu hata kutamani kubadili katiba ili aendelee japo hawezi kukubali. Hii inampa nafasi ya kuwapendekezea watanzania nani awe mrithi wake.
2) Mwendo wa Dr. Magufuli ana uwezekano wa kuwa na idadi ya watu ambao yeyote kati yao akichaguliwa atakuwa mteule wake. Mfano: (1) Jinsi ambavyo Naibu Speaker alivyoingizwa, sitashangaa kama 2025 atajitokeza kugombea. Akigombea baada ya kulelewa enzi hizi ngumu kutokuwa chaguo lake. (2) Tunamuona Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Daffo. Ukimuangalia sana, hatofautiani na Magufuli katika mambo Fulani. Matamshi yake hayaonyeshi ubandia au uigizaji wowote. Huyu namtilia shaka kuwa yuko analelewa. (3) Wakati watu waliposema Humphrey Polepole anapigania ukuu wa Wilaya niliwashangaa. Na naamini Polepole hakuwa na haraka ya kuupata Ukuu wa Wilaya. Kama angependa kupigania angeutafuta uwaziri. Kitendo cha kumteua kwa nafasi ambayo kimuonekano ni ya chini kwake sitafanya kosa nikisema amepelekwa kwenye nafasi hiyo ya chini ili apande polepole na kufikia 2025 atakuwa ameupata uzoefu ambao kwa sasa unaonekana hana na labda watanzania watakuwa wamemjua zaidi. (4) Kwa mwendo huu Magufuli anaweza kuweka chaguo lake hata chama cha upinzani ili mradi kufika siku zile atakayepita awe mmoja kati ya walengwa wake.
Kama huu nio mkakati wake basi Baada ya Magufuli umagufuli utaendelea. Kama hakuwa amekusudia hivyo nitashangaa sana kama hataanza.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments