DK. SLAA KAPASUA JIPU, KASHINDWA KULIKAMUA... KAKIMBIA!
Na Daniel Mbega
WASWAHILI wanasema, 'Msemea sikioni, siyo majinuni'! Maana yake ni kwamba, yeyote anayekunong'oneza kuhusu jambo fulani, katu siyo mjinga.
Septemba Mosi, 2015, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, aliibuka baada ya ukimya wa mwezi mmoja na kueleza msimamo wake katika siasa na mambo yaliyomfanya akimbie.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa muda wa saa 1:30 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa, pamoja na mambo mengine, alieleza namna mchakato wa kumkaribisha Edward Lowassa ndani ya Chadema na hatimaye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulivyogubikwa na hila kutoka kwa viongozi wa chama chake.
Aliwatuhumu viongozi wake hao kuuchakachua mchakato na hata hoja alizozitoa, ikiwemo kupewa orodha ya watu ambao Lowassa aliokuwa anakwenda nao Chadema, ilizimwa huku Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Profesa Abdallah Safari, akiichana barua yake ya kujiuzulu aliyomkabidhi.
Kubwa zaidi lililoleta mtikisiko ni maelezo ya Dk. Slaa kwamba, kumbe mchakato wote huo ulifanywa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ambaye Slaa mwenyewe anamwita 'mshenga'.
Alimnukuu Gwajima akimshawishi amkubali Lowassa kwa vile anakubalika na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kwamba maaskofu 30 kati ya 34 wa Kanisa Katoliki walikuwa wamelambishwa sukari guru na wanamkubali.
Hali hiyo ndiyo iliyozusha mtafakaruku mkubwa wa kisiasa ambao wapinzani waliuelezea kwamba una lengo la kuligawa taifa.
Slaa hakuwa majinuni alipotoa tuhuma hizo. Alikuwa sober, hakuwa amekunywa kileo wala hakuwa anaumwa, tena hakulazimishwa na yeyote… alimaanisha alichokuwa anakisema.
Hata hivyo, Septemba 8, 2015 Askofu Gwajima naye aliibuka kujibu mapigo ya tuhuma za Dk. Slaa, akisema kwamba Paroko huyo mstaafu wa Kanisa Katoliki hana hoja kwa sababu 'ametekwa na mkewe' ambaye alitamani sana kuwa 'Mke Namba Moja wa Tanzania' (First Lady).
Akasema, siku Lowassa alipopokelewa Chadema, Dk. Slaa alitupiwa nguo nje na mkewe na kwamba alilala kwenye gari huku kitendo hicho kikishuhudiwa na walinzi, ambao yeye Gwajima ndiye aliyempatia Slaa ingawa walikuwa wanalipwa na Chadema.
Gwajima ameruka futi 100 kwamba hajawahi kumweleza Dk. Slaa kwamba kuna maaskofu 30 waliohongwa, hivyo maneno hayo ni ya kutungwa.
"Dk Slaa anasingizia kuwa maaskofu 30 wamehongwa na Lowassa, hii ni kuwaondolea maaskofu kuaminika (credibility) ili waonekane kuwa hawafai," alisema Gwajima na kuongeza kuwa; "Maaskofu Wakatoliki hawakupewa rushwa, maaskofu wa KKKT hawakupewa rushwa, mimi sikupewa rushwa."
Ukiangalia mambo yanayoendelea unaweza kusema hizi ni ngonjera ama malumbano na majigambo, sanaa ambazo zimetoweka nchini mwetu kwa vile mitaala imebumundwa na wajanja na Kiswahili kinaelekea kupoteza misingi hata shuleni...
http://www.brotherdanny.com/2015/09/dk-slaa-kapasua-jipu-kashindwa.html

--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
www.brotherdanny5.blogspot.comINVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" ~ Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments