UCHAGUZI MKUU TANZANIA NA VITA YA MAFUTA NA GESI
Na Daniel Mbega
WIKI iliyopita nilikuwa napitia – kwa mara nyingine – kitabu cha Confession of an Economic Hit Man (Ushuhuda wa Mharibifu wa Kiuchumi) ambamo John Perkins, Mmarekani ambaye alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kufanya ulaghai wa kijasusi kuhujumu uchumi wa mataifa mbalimbali, hasa ya Dunia ya Tatu.
Perkins anasema katika Dibaji: "Waharibifu ama wapigaji wa kiuchumi ni wataalamu wanaolipwa fedha nyingi kuzihadaa nchi mbalimbali ulimwenguni na kuvuna matrilioni ya dola. Wanachukua fedha nyingi kutoka Benki ya Dunia, Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID), na mashirika mengine ya 'misaada' ya kimataifa na kuyaingiza taasisi kubwa na mifuko ya matajiri wanaomiliki rasilimali za dunia hii. Silaha zao ni kuangalia ripoti za kifisadi za fedha, chaguzi zenye utata, malipo yasiyo rasmi, utesaji, ngono, na mauaji. Wanacheza mchezo wa kale ambao umekuwa kama himaya, lakini ambao umegeuka kuwa wa kutisha hasa katika kipindi cha utandawazi."
Yapo mengi ambayo anayazungumza, lakini kubwa ni mbinu wanazotumia kuzirubuni nchi zinazoendelea (hii ikiwa na maana na Tanzania) ili kuchota rasilimali zilizopo.
Perkins, ambaye alikuwa jasusi wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), anasema mara nyingi wanachokifanya ni kwenda kutoa misaada na mikopo kwa nchi hizo kwa kujenga miundombinu ya barabara, viwanda, nishati na maeneo ya maegesho.
Mara nyingi, anasema, mambo wanayoyafanya yanakuwa yale ambayo yatawasaidia matajiri wachache na siyo wananchi walio wengi ambao hawapati umeme wala miundombinu mingine, kwa kifupi misaada hiyo haiwasaidii wananchi walio wengi.
Anasema, misaada na mikopo hiyo 'yenye masharti nafuu' kwa nchi hasa zenye utajiri wa rasilimali mbalimbali ikiwemo mafuta, inakuwa mikubwa na madeni yanazidi kiasi kwamba nchi husika inashindwa kulipa.
Ikishafikia hatua hiyo, anasema, wanarudi hapo na kuwashawishi viongozi wakisema: "Tazama, deni hili ni kubwa, hamuwezi kulilipa, tuachieni tuchimbe mafuta, madini au rasilimali nyingine muhimu kufidia deni hilo kwa malipo madogo sana".
huwezi kuwatambua waharibifu hao wa kiuchumi, kwa sababu ama wanaweza kuja kwa mgongo mwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ama maofisa waubalozi wanaofahamika kama Mwambata wa Kiuchumi (Economic Attache).
Katika baadhi ya mataifa, wanaposhindwa kufanikisha malengo yao kutokana na ugumu wa viongozi, wanaweza kuwatumia harakati za vyombo vya habari kueneza propaganda kwamba serikali fulani haifai, au la wanaweza 'kuwapoteza' (kuwaua) viongozi wanaoonekana kikwazo kwa kuwatumia wauaji ambao wanafahamika kwa jina la 'mbweha' (jackals) ambao nao huwa ubalozini kama maofisa wa usalama. Ikishindikana kabisa, basi hupeleka majeshi katika mataifa hayo.
Mbinu hizi hazitumiwi na na CIA peke yake, bali mataifa mengi yanafanya ujasusi wa aina hii wa kiuchumi kwa nia na madhubuni ya kukomba rasilimali za mataifa yanayoendelea huku wakija na kisingizio la misaada na mikopo kwa shughuli za maendeleo ya kijamii, mara nyingi fedha hizo huwa hazitolewi taslimu.
Nilikuwa napitia mistari mbalimbali kwenye kitabu hiki ndipo nikakumbuka kwamba deni la taifa hadi kufikia Desemba 2014 ni Shs. 27.04 trilioni (Shs. 20.23 trilioni ni deni la nje na Shs. 6.81 trilioni ni deni la ndani) ambapo kwa hesabu ya haraka, kila Mtanzania kati ya watu milioni 45, haijalishi kama ni mtoto au mzee, anadaiwa Shs. 600,000/-.
Japokuwa serikali inajipa moyo kwamba deni hilo asilimia 28, hivyo bado inakopesheka kwa kuwa kiwango cha ukomo wa kukopa ni asilimia 50, bado inatia mashaka kama linaweza kulipwa leo au kesho.
Tanzania ni moja ya mataifa yanayoendelea na yenye rasilimali nyingi ambazo kwa miaka mingi zinachotwa na kupelekwa nje huku Watanzania wakiwa hawanufaiki na wakiendelea kuogelea katika dimbwi la umaskini.
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) nayo ni mengi mno Tanzania, yapo yanayojishughulisha moja kwa moja na jamii, lakini yapo mengine ambayo kazi zao ni za kiharakati zaidi na hutegea kama kuna hoja yenye kutatiza na kutoa matamko ama kuhamasisha wananchi wapinge.
Kwa sasa Tanzania imekuwa kivutio cha uwekezaji kwa mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza, China, India na kadhalika.
Ugomvi mkubwa wa uwekezaji nchini Tanzania ni baina ya Marekani na China, ambayo inakuja kasi sana.
Marekani, ambayo ilikuwa inaongoza kwa uwekezaji, hivi sasa inashika nafasi ya tano nyuma ya Uingereza, China, India na Kenya.
Hadi kufikia mwaka 2012, uwekezaji wa moja kwa moja wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa Dola 950 milioni, wakati Uingereza ilikuwa inaongoza kwa kuwekeza jumla ya Dola 4.7 bilioni kutokana na makampuni ya BG Group Plc lililojikita kwenye gesi asilia na mafuta pamoja na kampuni ya SABMiller Plc, India ilikuwa imewekeza Dola 1.8 bilioni, wakati Kenya imewekeza Dola 1.5 na China ilikuwa imewekeza Dola 1.4 bilioni...
http://www.brotherdanny.com/2015/09/uchaguzi-mkuu-tanzania-na-vita-ya.html

--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
www.brotherdanny5.blogspot.comINVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" ~ Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments