[wanabidii] Wapumbavu na Marofa bye bye

Monday, August 24, 2015
Enyi wapumbavu na Malofa, jiandaeni kuhama nchi baada ya uchaguzi, vinginevyo, jela
 
    Hakika naiona Tanzania mpya baada ya uchaguzi wa Oktoba. Tanzania ijayo itakuwa mahala pabaya sana kuishi kwa wapumbavu na malofa.
 
    1. Kutakuwa na jela maalum kwa malofa na wapumbavu ambao siku zote wamekuwa wakituibia Watanzania. Mafisadi, majizi na mahujumu uchumi.
 
    2. Tanzania ijayo itaweka usawa baina ya wananchi. Hiyo itawanyima fursa mafisadi ambao wamekuwa wakitumia umaskini wetu kujitajirisha.
 
    3. Tanzania ijayo itakuwa ya viwanda. Wananchi wengi watakuwa busy na kazi hivyo itakuwa ngumu kwa wapumbavu na malofa kuwatumia Watanzania kama chambo kwenye maandamano.
 
    4. Elimu itakuwa bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Yale mafisadi yaliyotuibia yakajenga mashule yao yakawa yanatoza ada kubwa sasa hali itakuwa mbaya. Heshima ya shule za serikali itarudi tena.
 
    5. Enyi mafisadi, katika Tanzania ijayo, ili chama kiwe cha siasa lazima kiwe na sura ya kitaifa. Chama ambacho viongozi wake wakuu wanatoka kanda moja tu hakitapata nafasi ya kugombea
 
    6. Enyi wauza unga, Tanzania ijayo viwanja vya ndege na bandari vitakuwa havipitiki. Biashara yenu itaingia kirusi na hivyo hakutakuwa na fedha za kufadhili mafisadi kwenda Ikulu.
 
    7. Enyi malofa na wapumbavu, CCM kimezaliwa upya baada ya malofa, wapumbavu na wachawi kuhama chama. Waliobaki tunaserebuka na kucheza.
 
    8. Enyi mafisadi na malofa, mmekuwa mkihujumu sana hospitali za serikali kwa kujenga mafoka kando ya hospitali hizo. Mmekuwa mkihamisha dawa za serikali na kuuza kwenye maduka binafsi. Tanzania ijayo hakutakuwa na mwanya huo. Heshima ya hospitali za serikali itarudi tena.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments