CHADEMA walifungua milango ya uchukuaji fomu kwa Wanachama wao kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwania urais kupitia chama hicho.
Huu ni mtego ambao DR. SLAA aliwekewa na endapo angejichanganya tu na kuchukua fomu ANGEKATWA kama ilivyokuwa kwa LOWASSA kule CCM na hapo ingemuwia vigumu kujiondoa CHADEMA kwa kuogopa kuitwa mpenda madaraka.
MBOWE na kundi lake wakabaki wameduwaa. Magazeti yakabaki yanaandika "URAIS CHADEMA KAA LA MOTO".
Kuondoka kwa SLAA sasa ni mwiba kwa MBOWE, LOWASSA na CHADEMA kwa ujumla. Kuna uwezekano wa kuwa kama USAJILI FYONGO KABISA kufanywa na CHADEMA, kumuinga LOWASSA na kuondoka SLAA.
Sipati picha SLAA anasimama jukwaa tofauti na la CHADEMA kwa ajili ya kuomba au kumnadi mgombea asiye wa CHADEMA huku akitumia agenda ya ufisadi wa Lowassa kama turufu ya kuwauwa wapinzani wake.
Itakuwa haina tofauti na TIMU KAMA REAL MADRID KUMUUZA MCHEZAJI KAMA CHRISTIANO RONALDO KWA MANU HUKU WAKIMCHUKUA MCHEZAJI KAMA ASHLEY YOUNG HALAFU TIMU HIZO ZIKAKUTANA.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments