[wanabidii] Kura yangu

Thursday, August 20, 2015

On Thursday, August 20, 2015 6:39 AM, Paschal Leon <paschalleon@yahoo.com> wrote:


 Wandugu,

Nawasalimu wapenda Amani wote

Kwa mara nyingine tena nitapiga kura hapo 25/10/2015. Enyi wagombea, ili niwapigie kura hakikisha kwenye kampeni zako unazingatia yafuatayo:

1.    Unapenda Amani, si mtu wa kulalamika, ila unatoa suluhisho kwa tatizo
2.    Eleza sera za chama chako, usizungumzie kufanikia au kushindwa kwa mpinzani wako
3.    Eleza utakapoenzi muungano, usiwe chanzo cha kuuvunja ila kuuimarisha
4.    Eleza utakavyolinda rasilimali za nchi, madini, hifadhi za taifa, n.k
5.    Usiwe na jazba katika kujieleza, uwe na busara, mcha Mungu, sahau yaliyopita, anza ukurasa mpya
6.    Uwe mtu wa kujitegemea, usitegemee makundi kukubeba
7.    Mtu wa watu, mwenye kujua mazingira ya Mtanzania kuwa wengi ni masikini na kuwainua kiuchumi, hatua kwa hatua
8.    Mwenye kujali hali za wakulima na wafanyakazi, pia wale wadogo kama vile mama ntilie, bodaboda, machinga; n.k
9.    Mwenye kutia kipaumbele elimu kuanzia ya awali hadi vyuo ili baada ya miaka 20 ijayo tuingie kwenye uchumi wa kati. Elimu kwanza.
10. Asiwe na dalili za kulipiza kisasi; maana ataleta mgawanyiko katika taifa.
11. Anaye-enzi mazuri ya Baba wa Taifa
12. Anayeheshimu watu wote bila kujali hali ya mtu.

Asante 


Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments