[wanabidii] Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesi: Wapinzani Wanafahamu Ngoma Wanayoicheza?

Saturday, July 04, 2015
Kwanza, nieleze masikitiko yangu kwa mswada muhimu kama wa mafuta na gesi kuona unajadiliwa na kutaka kupitishwa pasipo na kambi ya upinzani. Kwa miswada muhimu kama hii ilihitaji sana michango ya watu makini kama akina John Mnyika, Tundu Lissu, Halima Mdee and in fact, hata ex-MP Zitto Kabwe! Lakini pamoja na yote hayo, naunga mkono miswada hiyo ya mafuta na gesi kusomwa sana badala ya kusubiria bunge lijalo!


Nianze hoja yangu kwa kusema kwamba, wakati tunawashabikia wabunge wa upinzani ambao walikuwa wanataka miswada hii isisomwe sasa, kwa upande mwingine tusisahau pia kwamba kuna madalali wazawa hapa nchini wanaojivika sura ya uzalendo ambao pia hawataki miswada hii isomwe sasa! Inawezekana kwa kujua ama kutojua, wabunge wa upinzani hapa wanacheza ngoma ya madalali hawa wakati mpiga ala akiwa haonekani! Si ajabu, miongoni mwao wapo wanaofahamu wapiga ala!

Nadhani wengi wetu tunakumbuka baadhi ya watu wanaojivika mwamvuli wa uzalendo ambavyo wamekuwa wakiupinga muswada huu, na kimsingi kwa sababu moja tu! Wakati serikali na muswada husika inataka TPDC ifanyiwe mabadiliko na iwe ndilo shirika litakalohusika kwenye suala zima la mafuta na gesi kwa niaba ya Watanzania kama ilivyo kwa nchi mbalimbali duniani, "wazalendo" hawa wanapinga suala hilo! "Wazalendo" wetu hawa wanataka Watanzania binafsi waruhusiwe kwenye shughuli za mafuta na gesi!

It sounds good na kinyume chake horrible! Hata hivyo, hapa niweke sawa jambo moja ambalo wazalendo hawa na vibaraka wao wamekuwa wakipotosha kwa makusudi ili mradi ionekane sheria hiyo haifai!

Si kweli hata kidogo kwamba sheria inakataza Watanzania kujihusisha katika biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi… narudia, si kweli! Mtanzania yeyote mwenye uwezo anaruhusiwa kushiriki kwenye biashara hii! Kinachogomba ni kwamba, wakati "wazalendo" wanataka Wazawa wapewe preferential treatment, yaani upendeleo maalumu, sheria inataka wadau wote washindane kwenye fair play ground… uwe Kaburu au Mpogoro, hakuna cha preferential treatment!

Ukiangalia kwa haraka haraka, na ndicho "wazalendo" hawa wamekuwa wakiwaambia wananchi, mtu unaweza kudhani kwamba hii serikali haijali wananchi wake! Pamoja na kwamba hivyo ndivyo inavyoonekana, ukweli ni kwamba uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya kuangalia historia ya huko nyuma ya "wazalendo" wetu hawa! Kwamba, unaweza kumpa preferential treatment Mzalendo X mwenye Kampuni Y kumbe behind the scene Mzalendo wetu huyo anamiliki ONLY 10% ya share za kampuni husika na 90% zinamilikiwa na wageni!

Na mbaya zaidi, unaweza kukuta "wazalendo" wengine wanapewa hiyo preferential treatment na kupewa vitalu vya gesi kwa bei chee kisha na wao wanakuja kuvipiga bei kwa wageni kama ilivyotokea kwenye vitalu ya uwindaji na madini! Na hapa niseme jambo moja kwa wale wasiofahamu taratibu za usajili wa kampuni!

Kwa sheria zetu, ili kuanzisha kampuni panahitaji kuwapo na at least 2 shareholders! Sasa kinachofanyika, ikiwa chige nina connection za hapa na pale, natafuta "wabia" kutoka ng'ambo kisha tunaingia "ubia" kwenye biashara ya uchimbaji wa mafuta na gesi kupitia kampuni inayoitwa Chige Oil & Gas Co. Ltd ambapo shareholders ni Chige 20% na John Smith (Mwingereza) 80%! Documents zikikaguliwa unakuta huo ni ubia wa Mtanzania na mgeni wakati behind the scene unaweza kuta hata hiyo 20% imetolewa na huyo mgeni ili kukidhi sheria husika! Hapo, Watanzania tutadanganyika kwamba kampuni husika ni ya Mtanzania mwenzetu akishirikiana na mgeni kumbe ukweli ni kwamba, ni fully or at least 90% inamilikiwa na mgeni… lakini huyu nae anataka upendeleo maalumu kv ni mzawa!! Kwa wanaofahamu undani wa biashara ya utalii Arusha, wanafahamu pia suala hili!

Unakuta mshikaji Mtanzania ana biashara mzuri sana ya tour operator ukimuuliza alikopata pesa anakumbia alipewa mtaji na demu wake wa kizungu kumbe nyuma ya pazia unakuta biashara hiyo si ya kwake lakini kwavile kuna baadhi ya biashara wageni hawaruhusiwi kufanya, ndipo unakuta wanatumia madalali wazalendo!

Kutokana na udanganyifu wa hapo juu unaotumiwa na Watanzania wenzetu, ndipo ikaamuliwa kwamba kwa Mtanzania binafsi anayetaka kujishughulisha na biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi basi asimame ulingo mmoja na wageni badala ya kutaka tumpendelee kumbe tunayempendelea ni mgeni anayemtumia Mtanzania!

Kipengele kingine ambacho wazalendo wetu wanakipinga kwa nguvu zote tena kuliko kipengele hicho hapo juu (cha kutowapa upendeleo) ni ile sheria inayosema TPDC ndiyo itajishughulisha na biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kwa niaba ya Watanzania!

Hapa ikumbukwe kwamba, makamapuni karibu yote yaliyo makubwa duniani yanayojihusisha na biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi ni mashirika ya serikali! Na serikali ya Tanzania inataka kufuata mkondo huo huo wa kuiwezesha TPDC ndiyo ijishughulishe na biashara hiyo kisha iuze hisa kwa wananchi na hivyo kutoa fursa hata kwa wananchi wa kawaida kumiliki uchumi wa mafuta na gesi! "Wazalendo" wetu hawa hawaitaki kabisa sheria hiyo na wanataka TPDC isijihusishe kabisa na biashara hii kwa ile wanachosema TPDC ikijihusisha na biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi basi watadumaza ukuaji wa sekta binafsi na kwamba serikali itakuwa inakiuka kanuni ambayo walijiwekea ya kutofanya biashara!

Mwenye macho haambiwi tazama na ikiwa kusoma hatujui basi angalau tujitahidi kuangalia michoro ya picha ukutani! Hivi ni Watanzania wangapi wana uwezo wa kufanya biashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi?

Hivi wanapotokea watu kwamba hawataki TPDC ijihusishe na biashara hii ili hatimae iuze hisa kwa wananchi; hivi kweli watu hao wanatetea maslahi ya wananchi walio wengi au wanatetea maslahi yao binafsi? Na haishangazi hata kweny michango ya wabunge leo hii, Mtemi Andrew Chenge ni moja ya wabunge waliopinga baadhi ya vipengele vya mswada huo!

Kutokana na ukweli huo, utagundua kwamba hawa Watanzania wenzetu wanaojifanya eti ni wazalendo ndio wanaotaka miswada hii isubiri bunge lijalo kwa sababu wanafahamu bunge lijalo litakuwa na rais mwingine na hivyo huenda wakacheza karata za kusababisha sheria hizo zibadilishwe ili ziwe kama wanavyotaka wao! Remember, Rais Kikwete na ubaya wake wote ndie anayelipa uzito suala la TPDC ndiyo ifanye biashara kwa niaba ya wananchi! Na kutokana na ukweli huo, I bet JK ndie anashinikiza miswada hii ifanyiwe kazi sasa kwa hofu kwamba huenda rais ajae akafuata matakwa ya "wazalendo!" wetu hawa na hivyo sheria kubadilishwa! Wazalendo hawa walishangilia sana baada ya Muhongo kupigwa chini huku wakisahau kwamba kiburi cha Muhongo kilitokana na back up ya JK!

Kutokana na ukweli huo, utagundua kwamba kuna hatari kubwa kwa maslahi ya wengi endapo miswada hii itasubiria bunge lijalo kuliko kama itasomwa hivi sasa na kufanyiwa maamuzi ya busara hivi sasa!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments