[wanabidii] Boss Mkuu wa Usalama wa Taifa Rwanda Emanuel Karenzi Karake Akamatwa London

Tuesday, June 23, 2015

MKUU WA USALAMA WA TAIFA WA RWANDA AKAMATWA UINGEREZA !


London,Uingereza,

Mkuu wa usalama wa taifa wa nchi ya Rwanda Major Gen.Emanuel Karenzi Karake amekamatwa na wanausalama katika uwanja wa ndege wa Heathrow nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita,kwa kutuhuma za mauaji ya kivita mwaka 1994 na baada ya mwaka huo pia.Major Gen.Karenzi Karake aliwekwa kizuwizini na baadaye  kufikishwa katika mahakama ya Westminister,amri ya kukamatwa kwa mkuu huyo wa idara ya ujasusi (NISS) ya Rwanda kunatokana na ombi la mahakama ya nchi ya Spain ambayo imeorodhesha watu wapatao 40 kuhusika na makosa ya kivita nchini Rwanda ,mashataka yalifunguliwa 2008 kufuatia uchunguzi uliofanywa na kikosi cha mahaka ya spain kinachoongozwa na Andreu Melles .
Mkurugenzi mkuu huyo wa usalama wa taifa wa Rwanda Bw.Karenzi Karake mwenye umri wa miaka 54 bado yupo kiziwizini na anatagemea kupandishwa Kizimbani tena siku ya Alhamisi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments