[wanabidii] Barua ya Wazi Kwa Ndg. Hamis Kigwangala

Tuesday, May 26, 2015

Barua ya Wazi Kwa Ndg. Hamis Kigwangala

Mhe Kigwangala;

Nilipata wakati mgumu sana kufikiria maneno mazuri na mepesi yatakayoweza kukusaidia kuelewa mantiki ya barua hii nikaona naweza poteza muda bila kusema chochote na hivyo kuamua kuandika yale ambayo nafsi yangu yataridhika kwayo.

Nimesoma andiko lako sana, juu ya Ndgu Edward Lowassa nimelipitia kwa kadri ya uwezo wangu na kwa namna ambayo ufahamu wangu ungeweza kunipa tafsiri chanya ila kumbe nimekuja kugundua kuwa kumbe si mimi tu wako wengi waliokudharau wewe na hicho ulichokiandika.

Hamis Mtanzania yeyote angeuliza wewe na Edward mnakutana wapi hata kuja na andiko hilo la kikuwadi. Lakini wengine wangeuliza hayo yoote umekuja kuyajua baada ya kutambua kuwa unautaka Uraisi usioupata ama baada ya kugundua kuwa hata hicho kitumbua ulicho nacho sasa kinaelekea kujaa mchanga?

Hamis wewe bado ni kijana hivi vita unavyodhani unapambana na Edward wenye akili ambao wala hawana Degree uliyo nayo wewe wanajua kuwa tatizo lako si Uraisi bali ni "Uoga" wa kutumbua chako kuingia mchanga.

Vijana wenye kuhitaji nafasi kama hiyo unayoitaka (ndoto za alinacha) wako wengi na wanajaribu ama kujitahidi kujijenga ila wewe unadhani wa kukujenga ni Edward kwa kuandika upuuzi usio na staha kwako wewe na hata hao unaowaongoza.

Hamis tambua hili haki huchelewa lakini ni lazma itafika; usihofia sana kuona haki ya yule anayepaswa kukamata nafasi hiyo iliyo nayo imeshafika bali hofia ni kwa nini ulidhani kuwa haki hiyo haikuwa yake.

Lakini Hamis nimebahatika sana kupitia baadhi ya kukarasa katika Kitabu chako lakini mtu yeyote angeshangazwa kwa namna ambavyo mzazi wako mmoja hakuwa na nafasi yeyote katika Kitabu hicho.... Sasa hivi kweli kama umeutenda mti Mkavu hivyo sembuse Mti mbichi??

Tanzania inajua na Dunia inajua Vita unavyojifanya kupigana wala si vya Edward na Edward mwenyewe tunamjua anavyojua kupuuza na ni wito wangu kwa wale wote wenye imani chanya na Edward kwamba Wakupuuze wewe kuliko Upuuzi wenyewe.......

Huna sifa iwayo yoyote ila kujibiwa ila nimefanya hivi ili utambue kuwa yumkini kuna laana ya mzazi wako inakutafuna hivyo rudi ukatubu haijalishi alikutupa ama kukutelekeza bali bado amri za Mungu ziko pale pale.

Usijifanye unajua sana kuhusu Richmond zaidi ya kina Lembeli na kina Sendeka lakini hao hao ndio leo wameona kulikuwa kuna dosari ktk hilo......

Tafiti upya namna utavyoweza kutoka na si kwa kushindia uji wa matanga.

Nikutakie heri ktk maisha yako ya Ustaafu ukiwa na umri huo ulio nao; Nyumba ulipewa ukawa mpangaji usiye na fadhila hivyo mwenye nyumba kaamua kurudi tena kirahisi manake kasikitishwa sana kwa namna ambayo umetaka hata kubadilisha mikataba na kutaka Kumiliki nyumba hiyo.......

NB; Unapopewa lifti usithubutu kujaribu kupiga honi mwache mwenye gari aendelee na majukumu yake....

Tarehe 30.05.2015 kuwa tayari kusoma namba za soli......

Meitinyiku Robinson

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments