[wanabidii] MAKUNDI YA WABUNGE NDANI YA BUNGE LETU

Thursday, January 22, 2015
NIMEJIFUNZA kitu jana kuhusu makundi ndani ya Bunge letu bila kujali walio mawaziri au manaibu.Kundi la kwanza ni la Wabunge watu wazima waliokaa Bungeni muda mrefu kidogo kundi hili ni la akina Anna Makinda na Wabunge wengine Wazee wa Chama tawala. Hili kundi ndilo kundi kuu hawa wanajuana walikotoka interests zao mpaka makando kando yao. Wanajua mbinu zote za kurudi Bungeni upya wanajua namna ya kucheza karata vema kwa wapiga kura wao na ukichangia kiukibaraka kwa kutumwa na matajiri wa nje wanajua wanajua kwasababu na wao walishawahi kutumika. Wamechoka hawana haja tena hata ya uwaziri wao ni bora siku ziende. Kundi la Pili nalo ni la Wazee bila kujali itikadi humo unawakuta Ndesamburo Wassira Shekifu hawa wanateteana kwa Uzee wao pale maslahi ya Wabunge Wazee bila itikadi yakiguswa. Kundi la tatu ni la kinamama Wazee wa CCM hawa ni Anna Abdallah ni Wenzie wao huamini kuwa ndio mzizi hasa wabunge kuwa na idadi kubwa ya akinamama na ni wakali ukigusa maslahi yao na pia huungana na akina Mama wa Upinzani pale Mwanamke akidharirishwa. Kundi la tano ni Wabunge vijana wa CCM akina Ridhiwan Magige Bulaya na Wenzie hawa wanaamini wao ndio chachu ya Wanasiasa vijana kwa Chama tawala na huongoza misimamo ya maslahi ya vijana ndani ya vikao vya Caucus ili kuwafanya Wazee wasiwadharau kuona ni wachanga.Kundi la sita ni Wabunge Vijana bila kujali itikadi hawa ni akina Nasari Ridhiwan Mdee,Mkosamali Magige Mgimwa na wenzie hawa kauli mbio yao ni moja kuwa vijana kwanza kwa Tanzania mpya bila kujali itikadi ya kivyama wanaongoza mijadala wanasimamia masuala mazito yenye muktadha sahihi wa maendeleo ya nchi humu utakuta wanaolipuka kwa ukali bila itikadi ni Filikunjombe, Mnyika Bulaya na Mkosamali Mdee na Zitto. Uzuri ninaouona ktk kundi hili huwa hawapondani wanapotembelea majimboni kwao. Mfano Nassari aligoma kwenda kupiga kampeni Chalinze na pia aligoma kwenda kwa Mgimwa kupiga kampeni na ni kwa ombi maalum la wabunge hao wenzie vijana ili Bunge lijae vijana. Hii ni safi sana. Kundi saba ni la wabunge majeruhi waliokuwa mawaziri mawaziri wakuu au manaibu wakajiuzuru kwa kashfa mbali mbali au kuondolewa tu katika cabinet. Hawa hawana matumaini ya kurejea kuwa mawaziri hawana mawasiliano ila wana hasira wakipata mwanya wa kuibonda serikali wanaibonda kisawa sawa hawana cha kupoteza mwaziri huwa wanawaogopa sana. Kundi la mwisho ni kundi baya sana hili ni kundi la BUNGE ZIMA ni kundi baya kwasababu wanatofautiana kiupinzani kwa itikadi zao na huwa wanapambana kweli hadi wakati mwingine kutukanana na kashfa lakini siki utapokuja muswada wa kupunguza mishahara ya wabunge ili zijenge maabara hapo wataungana wote bila kujali CCM au UKAWA kupinga muswada huo kwa nguvu. Kichekesho ni pale Tundu Lissu anapopambana Mama Makinda vikali halafu usiku wakati wa tafrija ya Wabunge nyumbani kwa PM Pinda wanafungua wote muziki wa Jojina. Nafikiri kundi hili likiondolewa TBC1 live waendeshe Bunge bila TV Bunge litakuwa kama lile la Nyerere pale Karimjee enzi za Ikarus na KAMATA.Tatizo TV zikiwangalia wanageuka akina Ray na Kanumba zisipokuwapo watakuwa wao halisi. Ukitegemea mwanasiasa akiletee Maendeleo yako binafsi umekwisha kula mahali ulipo hata kwa trafiki siku hizi slogan sio usalama wa barabarani ni usalama wa matumbo yao kwanza. Wasalam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments