[Mabadiliko] Mwaka 1964 Ulikuwa Mgumu Kwa Nyerere Katika Kipindi Chote Cha Uongozi Wake

Wednesday, January 21, 2015


Ndugu zangu,

Nimefurahiwa na mwitikio chanya wa simulizi za kihistoria nilizozianzisha jana. Nawashukuru wote mliochangia. Ni imani yangu, kuwa ni kwa namna hii tunaweza kuipitia historia yetu na kuihifadhi kwa vizazi vijavyo pia. Itawasasaidi Watanzania wa kesho na keshokutwa kujitambua.

Ndugu zangu,

Ni bahati mbaya kuwa muda ni mdogo sana wa kusimulia mengi, ambayo, baadhi yetu tumepata bahati ya kuyasoma au kusimuliwa moja kwa moja na waliokuwepo.

Naahidi kuendelea kuwaletea, hata hayo machache, kila nitakapopata muda. Nitafanya hivyo ili kulifanya jukwaa hili kuwa darasa hai la sote kujifunza. Ngoja sasa niendelee na nilichoanza kusimulia jana.

Unabaki kuwa ni ukweli wa kihistoria, kuwa mwaka 1964 ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa uongozi wa Julius Nyerere kuliko wakati mwingine wowote. Kulikuwa na matukio makubwa yaliyomtikisa Julius Nyerere na Tanzania kama taifa changa.

Tumeona mifano ya Mapinduzi ya Januari 12, Zanzibar na Army Mutiny ( Uasi wa jeshi) wa Januari 20, 1964. Siku kama ya jana.

Ni katika mwaka huo, Wachina na WaCuba waliingia kwa kasi Zanzibar mara baada ya Mapinduzi. Hali hii iliwatisha Wamarekani. Ikaja taarifa ya kupandikizwa ya kiintelijensia. Ni katika miezi hiyo hiyo. Kwamba Marekani na Uingereza wanapanga njama za kumwangusha Karume. Nyerere akaridhia Karume amfukuze Balozi Mdogo wa Marekani kutoka Unguja.

Julius Nyerere akagundua baadae kuwa alikosea. Akaenda mwenyewe kwa Balozi wa Marekani kufafanua kilichotokea.

Kwenye telegramu ambayo Balozi wa Marekani aliituma White House na CIA Januari 1965 , Balozi huyo, Bw. Leonhart anauelezea mkutano wake na Julius kwa kusema, " Haukuwa mzuri…."

" Nyerere bekglagade djupt att han kunde inte andra sitt beslut"- ( Swedish) Kwamba Nyerere alisikitika lakini hakuwa tayari kubadili uamuzi wake ( Kumfukuza Balozi mdogo wa USA) ( Pa Vag Mot Presidenten, Ukurasa wa 196)

Mengine yaliyojiri kwenye mkutano wa Julius Nyerere na Balozi Leonhart ni vema yakabaki kwenye maandishi ya mwandishi Holmqvist na kwa lugha yake, maana, kuyaweka bayana hapa haiwezi kuwa ni kwa maslahi ya taifa letu.

Nikipata muda nitawasimulia mengine kutoka kwenye kitabu hiki. Bahati mbaya, kitabu cha Holmqvist hakipatikani kwa lugha ya Kiingereza, Lakini, mengine anayosimulia Holmqvist unaweza pia kuyapata kwa lugha ya Kiingereza kwenye vitabu vya waandishi kama ( The Critical Phase in Tanzania 1945-68:Nyerere and the Emergence of a Socialist Society, Cranford Pratt ) , ( Nyerere of Tanzania, William Edgett Smith) na hata( The Dark Side Of Nyerere's Legacy, Ludovick Mwijage) Hiki kimepigwa marufuku.

(Ninanavyo vitabu hivyo na vinginevyo kwenye maktaba yangu kwa anayetaka kuniazima)

Siku Njema.

Maggid,
Dar es Salaam.

http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye5khbCHtZM1NCp5qk_A7T1g7asMLPVkr-v4ZwtkJ4PRHQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments