Hiki ni kilio kikubwa sana Huku Kimara na Jimbo lote ta UBUNGO. Ni takribani siku ya Ishirini na Tisa leo HAKUNA Maji. Cha kushangaza sana, Hakuna Taarifa kwenye Vyombo vya Habari(TV, Magazeti au Mitandaono) wala PA kusikika Barabarani. Ina sikitisha kwa kweli. Nimefanya Survey Jana, Debe/Dumu moja la lita 20, sasa Linauzwa Tzs.1,000/- hadi Tzs.1,500/- kwa maeneo ya SUCA, KIMARA, BARUTI, Manzese na Magomeni Kagera. Watu wana taabika sana, wanakesha kusaka maji.
Wakati, Ofisi za Wizara ziko katika Jimbo jilo, hakuna hata anayeguswa kushughulikia Kilio hiki....Inasikitisha kwa Kuwa Hapo Jirani na Tank Kubwa Ubungo, Kuna Kiwanda cha Kufyatua Matofari, kinatumia Maji BURE, Pamoja na Wakubwa wa Wizara Kumkamata Mhusika, lakini hakuna mabadiliko.
Mheshimiwa, Waziri Jumanne Maghembe Unaelewa hayo??? Ni kwa nini swala la Maji UBUNGO ninafanyiwa Mzahaa na kuingizwa SIASA???. Inasikitisha zaidi, kwani Wenye Magari ya Maji Imekuwa neema kwao, na Maji ya kwenye hayo magari yana chumvi Kupindukia.
DAWASA/DAWSCO Hivi Ni lini hasa Mtatenga Pembeni Siasa na Uhalisia wa Maisha ya Wananchi hawa wanao teseka na Uhaba wa Maji katika Kipindi hiki cha Jua na Joto Kali Dar Es Salaam????
Kwanini Bomba hilohilo la Ruvu, kuna Sehemu nyingi tu zinaendelea Kupata Maji, na Kwanini Wananchi wa Kimara, Ubungo na Manzese tu???
Jiandaeni kujibu hoja kabla hujuma zenu hajijawekwe Hadharani.
Mwaisho namalizia Kwa Kumtaka Waziri wa Maji afike mwenyewe ajionee wananchi wanavyo taabika.
Wenu mwanabidii.
Mwasajone
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments