[wanabidii] CUF INALAANI FITINA ZA KUIGAWA UKAWA UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAJUMBE WA UKAWA

Tuesday, December 09, 2014
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYOMBO VYA HABARI[/B][/U]

CUF INALAANI FITINA ZA KUIGAWA UKAWA UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAJUMBE WA UKAWA

• DAVID KAFULILA NI MWEREVU HAKUPASWA KUTOA KAULI KAMA HIYO

• CUF TUMESHINDWA KUVUMILIA, TUNALAANI KAULI HIYO NA ILE YA MAKAMU MWENYEKITI WA BAWACHA

NDUGU, Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini, Chama Cha Wananchi CUF kinapenda kutoa tamko rasmi la kulaani viongozi wa Vyama vya CHADEMA, NCCR na hata Taasisi ya TWAWEZA kuhusu kauli zao juu ya Mgombea wa UKAWA kwenye Uchaguzi wa Rais 2015. Kutajwa kwa Jina la DR. SLAA kwa kisingizio cha Utafiti au maoni binafsi ya Viongozi wa Vyama hivyo na Taasisi ya TWAWEZA sio tu ni kinyume na utaratibu za UKAWA lakini pia ni mpango maalum wa kusambaratisha Umoja huo.

CUF ni miongoni mwa Vyama vinavyounda Umoja huo, hatujawahi kutoa kauli yoyote juu ya Mgombea tunayedhani anafaa kugombea kupitia UKAWA kwakuwa tunaamini muda haujafika. Kufanya hivyo kwa utashi wa mtu au kwa misimamo iliyojificha ni kuhatarisha Umoja huu. David Kafulila ni Mkurugenzi wa Habari wa NCCR ni Mtu mwenye ufahamu wa kutosha na anaweza kupima athari ya jambo analolitolea maoni, kwa hivyo kama Kiongozi alipaswa kufahamu athari zitakazojitokeza kutokana na kauli yake.

Ndugu wanahabari Mtakumbuka Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) uliundwa kupitia wajumbe wa Vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR na NLD ikiwa na lengo la kutetea maoni ya wananchi yaliyowasilishwa katika Rasimu ya Katiba na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoratibiwa na Jaji Mstaafu Joseph Warioba.

Kupitia Umoja huu ambao Wenyeviti wa vyama vyetu walishiriki kikamilifu kusimamia maoni ya wananchi ambayo serikali dhalimu ya CCM ilitaka kuchakachua maoni ya wananchi.

Ndugu wanahabari na watanzania wote ni mashahidi kuhusu kazi kubwa iliyofanywa na viongozi na wajumbe wa UKAWA katika mchakato wa Katiba,kupitia umoja huu hulka kuungana kwa lengo la kuwaondoa CCM ilivyozaliwa.

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kuwa ni miezi minne imepita mara baada ya kusaini makubaliano ya ushiriki wa pamoja wa vyama vinavyounda UKAWA kuanzia uchaguzi wa serikali za Mitaa na kuendeleza mikakati na majadiliano ya kusimamisha mgombea mmoja wa Urais hapo mwakani ambapo mazungumzo ya mashirikiano yanaendelea.

Tangu kutangazwa kwa makubaliano hayo,zimezushwa kauli mbalimbali zenye lengo la kupotosha dhamira ya dhati ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ikiwemo hili la kutajwa kwa Mgombea wa Urais wa(UKAWA).

TUNALAANI VIKALI kuenezwa kwa taarifa za uteuzi wa Dk.Slaa kama Mgombea wa Umoja huu na tunapinga kuendelea kuenezwa kwa habari hizo kwani mashauriano ya ushirikiano wa masuala mbalimbali ikiwemo Mgombea Urais yatajadiliwa kwa kadri muda utavyohitaji kufanya hivyo.

Tunalaani kitendo Cha Mbunge wa Kigoma Kusini,David Kafulila na Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA kumtaja Dk.Slaa kama Mgombea wa Urais,tunahitaji waeleze ni kikao gani walichoshiriki katika kutoa uamuzi wa uteuzi huo.

Tunaamini kuwa kama ni maoni yao binafsi walipaswa kuzungumza katika vikao vya vyama vinavyounda UKAWA na sio kuzungumza katika vyombo vya habari kama walivyofanya Kafulila na Mwenyekiti wa Bawacha.

CUF tunaamini kuwa huu ni mwendelezo wa sumu iliyoanzwa kupandikizwa na ripoti ya Utafiti wa Twaweza kuiaminisha jamii kuwa mgombea wa Ukawa ni Dr.Slaa.

CUF kinalaani vikali mwendelezo wa viongozi tena wanaounda UKAWA kuzungumza UONGO wa wazi bila kujali ushiriki wa vyama vyao katika UKAWA kwani taarifa hizi zina lengo la kuwachanganya watanzania ambao wanahitaji mabadiliko .

Tunahitaji vyama ambavyo wagombea wake waliotoa kauli hizo zilizoripotiwa na vyombo vya habari kupewa onyo na kuwahitaji kukanusha wenyewe kupitia vyombo vya habari .

Tunawataka watanzania na wanachama wa CUF kuzipuuza taarifa hizo ambazo lengo ni kuwagawa watanzania waliochoshwa na serikali isiyowajali wananchi.

Tunaamini kuwa Ukawa itaendelea kupigania nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania hivyo tunawahitaji wanachama wa CUF na watanzania wote kuwa watulivu na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

CUF tunasema ni mapema mno kufikiria mgombea wa Urais kabla ya kuweka misingi imara ya mashirikiano ambayo inaendelea hadi sasa,tunawaomba watanzania kuzipuuza taarifa hizi
Imetolewa na;

Abdul Kambaya,
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF,
Jumatatu Desemba 08,2014,
Simu Namba; 0689609666.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments