[wanabidii] Taarifa kuhusu maendeleo ya afya ya Rais Kikwete

Wednesday, November 12, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostate Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.
Rais Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.

Aidha, Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.

Wakati huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.

Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments