[wanabidii] Mahututi aliyekimbiwa na mwanamke 'guest' afariki

Wednesday, November 12, 2014
Mtu mmoja amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kukutwa hali mahututi katika nyumba ya kufikia wageni.

Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Kassim Rashid (55) mkazi wa Ghana, Mbeya alifariki dunia wakati akitibiwa katika hospitali hiyo ya rufaa tarehe 10 Novemba 2014 mwendo wa saa kumi alasiri.

Taarifa ya Polisi kutoka mkoa wa Mbeya imesema kuwa awali majira ya saa tatu asubuhi, marehemu alifika kwenye nyumba ya wageni iitwayo Atukuzwe iliyopo eneo la Soko Matola akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambaye hata hivyo hakuweza kufahamika mara moja jina na makazi yake, na kuchukua chumba namba 6 na baada ya takriban dakika 20, mwanamke huyo alitoka chumbani humo na kwenda kusikojulikana.

Majira ya saa sita mchana, mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni, Nickson Kahanga (24) wakati anapita kuelekea uani, alisikia kelele za mtu akikoroma katika chumba hicho na alipofungua mlango, ndipo alipomkuta Kassim akiwa amejifunika blanketi mwili mzima akiwa mahututi.

Imeelezwa kuwa taarifa zilifikishwa polisi Kati na mhanga alikimbizwa katika hospitali ambapo muda mfupi baadaye alifariki.

Uchunguzi zaidi kuhusian ana tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuufanyia uchunguzi wa kitabibu mwili wa marehemu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments