Edward Lowassa ndio waziri mkuu aliewai kukaa katika kiti cha uwaziri mkuu kwa muda mfupi zaidi kuliko waziri mkuu yeyote yule; sasa angalia hii record yake ya kushangaza!!!!
One,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha nia ya dhati kukabiliana na foleni ya jiji la dsm; ambalo kimsingi ni kama jinamizi kwa sasa!!!!
Two,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana. Pale Bandarini kulikuwa na watu waliokuwa vibarua kwa muda wa zaidi ya miaka 15 lakini alipoingia uwaziri mkuu, ile hali kaisimamia jamaa wale wakapa mkataba wa kudumu.
Three,
Ndani ya muda mfupi alionyesha kujali elimu kwa wananchi. Hizi shule za kata ambazo ndizo zinazosaidia wananchi kuamka kwa sasa ni matunda ya Lowassa.
Four,
Tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Akiwa bungeni mara nyingi amekuwa akiongelea suala hili la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kiasi kwamba ilibaki kidogo tu ingekuwa malalamiko ya mikopo kwa wanafunzi ingekuwa historia.
Five,
Wakati akiwa waziri mkuu, kwa muda mfupi sana ilionekana kuwa uchumi sasa utapaa; na tayari kulikuwa na indicators za kutosha kuashiria hilo
Six,
Kwa muda mfupi sana utendaji serikalini ulikuwa unaenda kwa kasi ya ajabu. Kuanzia mdogo hadi mkubwa.
Seven,
Kwa muda aliokaa hajawahi hata mara moja kutoa kauli tata za kuashiria ubabe kwa wale wanaopingana naye. Kauli zake siku zote zimekuwa very straight kuwakabili watumishi wazembe na watendaji wanaotenda kazi katika mfumo wa business as usual.
Eight,
Ndio kiongozi pekee serikalini ambae ana record ya kutoa individual support kwa mwananchi mmoja mmoja pale atakapobaini kuwa panahitajika support kwa ajili ya huyo mwananchi. Hata bbc swahili walishawahi kuripoti kuhusu hili.
Nine,
Akiwa waziri mkuu alimbeba sana Kikwete kwenye utendaji wa kiserikali! Hadi sasa Kikwete amekata tamaa kabisa na mambo ya serikali. Anatamani siku anarudi toka maryland akute tayari 2015 imefika maana hana hamu kabisa na mwenendo wa mambo ndani ta taifa hili.
Ten,
Kikwete hatakaa amsahau kwa kumpoteza katika utendaji wa serikali yake. Na ndo maana uchaguzi wa 2010 Kikwete alipata shida sana! Na hadi leo anamlilia sana, ila mfumo wa chama chake unamgandamuiza sana.
etc,
HAYA SASA
Kuna waliokaa kwa muda waliokaa waliishia kuwaambia wafanyabiashara ukitaka mambo yako yawe mazuri jiunge na ccm!!!
Kuna waliokaa kwa kipindi walichokaa lakini kwa muda mfupi sana walionekana mara kidume kinalia bungeni, mara katoa kauli tata za kuwatisha wapinzani; eti wapigwe tu. Uwapige wapinzani ili iweje?
Hii nchi ya kwako peke yako?
Ahsanteni wakuu
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments