Re: [wanabidii] Uchambuzi wa habari: Wahisani kuzuia misaada kunawaumiza wanyonge..

Monday, November 10, 2014
Majid! Are you serious?
Yaani nchi wahisani wanatusaidia kwa sababu hatuna fedha. Wakati tukisubiri misaada yao mbunge wetu anagundua kuwa fedha zetu wenyewe zimeibiwa. Anabishiwa na kukejeliwa na mahala pengine kutishiwa. Anakazana mpaka wanaombishia na ndio wana mamlaka wanazidiwa wanaunda tume. Fedha zinalalamikiwa kwa kuibiwa kipuuzi tu.
Fedha zinazolalamikiwa kuchezewa zingeweza kupunguza mahitaji yetu.

Sasa watu wazima wanaliona na kuamua kusimamisha misaada yao mpaka tuonyeshe matumizi bora ya zile zetu wenyewe
Halafu unawakasirikia? Kwa kutaka uwe na akili siku moja usaidie wengine?
Sielewe
--------------------------------------------
On Sun, 11/9/14, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Uchambuzi wa habari: Wahisani kuzuia misaada kunawaumiza wanyonge..
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, November 9, 2014, 11:12 AM


Ndugu zangu,


Naungana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoitoa
Bungeni
Dodoma Alhamisi, Novemba 6, 2014, kuonyesha masikitiko yake
na ya nchi
yetu kwa ujumla kwa kitendo cha kuzuia misaada cha wahisani
kutoka nchi
za Jumuiya ya Ulaya ikiwamo pia Norway, Canada, Japan, Benki
ya Dunia na
hata Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Kama ilivyo kwa mwanadamu, hakuna duniani taifa timilifu.
Sakata la tuhuma za wizi wa fedha za Escrow/Iptl ni '
msiba' wetu Watanzania.

Lakini, kama nchi, Serikali yetu haijakunja mikono na
kusema ni ' Kazi ya Mungu tu'.


Watanzania tunaona na wahisani pia wanaona, labda kama
hawataki kuona,
kuwa Serikali iliiagiza CAG na Takukuru kulifanyia uchunguzi
suala hilo.

Sasa kabla ripoti hazijawekwa mezani na kuona hatua gani
wahusika
wanachukuliwa, tunashuhudia wahisani wakisitisha kutoa
kwenye bajeti
kuu, kiasi cha dola za Kimarekani 558 sawa na shilingi
bilioni 937.


Ni fedha nyingi mno kwa nchi kuwa na nakisi nayo. Kuwa
muhisani ni
pamoja na kumuheshimu unayemuhisani. Kwamba naye ana
wanaomtegemea ili
nao waishi na waendeshe mambo yao ya msingi ya kila siku.


Inavyoonekana, Wahisani wao wanaamua bila kufanya mazungumzo
ya kina na
wanaowahisani. Laiti Wahisani wangekaa chini na Serikali
kuzungumzia
azma yao ya kusitisha misaada yao kwa bajeti kuu, naamini,
kuwa
wangepata ufahamu mkubwa juu ya mchakato wa sakata hilo
ulivyo, na
kwamba wangevuta subira kusubiri matokeo ya mchakato huo. Na
katika
kipindi hicho bado wangetoa fedha walizotuahidi kama nchi
ili ziweze
kuchangia kwenye kuhakikisha watu wetu wanaendelea kupata
huduma za afya
na pia watoto wetu wanaendelea kupata elimu.

Hakika,
unapotembea vijijini na kukutana na picha kama hiyo hapo juu
ya watoto
wa wanyonge wa Tanzania kule Bigwa milimani, mkoani
Morogoro, wakiwa
wameamka alfajiri kuwahi shuleni, pengine bila kupata
kikombe cha chai
nyumbabi, basi, unajiwa na fikra, kuwa ni kwanini makosa
yenye kutendwa
na wachache katika nchi ipelekee wahisani kufanya maamuzi
yenye
kuwaumiza wengi wasio na hatia, na hata kuharibu mustakabali
wao
kimaisha, kwa kuwakosesha huduma bora za afya na elimu
bora.
Hivyo,
naungana na Waziri Mkuu wetu, Mizengo Pinda katika kukosoa
hatua ya
wahisani ya kusitisha msaada wao kwenye bajeti kuu ya
Serikali kwa
sababu za kutaka kwanza kuona hatua za Serikali juuu ya
sakata la
IPTL/escrow. Na hili la wahisani, linatukumbusha umuhimu wa
kujitegemea
kama nchi. Tupambane na mafisadi wetu kuhakikisha kuwa
hawaendelei
kutafuna vya kwenye hazina yetu.
Maggid,
Iringa.
http://mjengwablog.com




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments