[wanabidii] NANI APAZE SAUTI JUU YA UNYAMA ULIOFANYIWA MAREHEMU BETTY NDEJEMBI?

Sunday, September 14, 2014

NANI APAZE SAUTI JUU YA UNYAMA ULIOFANYIWA MAREHEMU BETTY NDEJEMBI?
Ni zaidi ya wiki sasa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wengi tu walijaribu kupaza sauti juu ya kifo cha utata cha binti mdogo marehemu Betty Ndejembi aliyekutwa na mauti baada ya kufanyiwa vitendo viovu vya kulawitiwa na kisha kutupwa mtaloni kabla umauti haujamkuta ktk hospital ya taifa Muhimbili.

Japo kuwa hakuwa mtu maarufu sana ila watu wanaofutilia mambo ya mitindo kwao jina la Betty Ndejembi halikuwa geni sana na kwa wanasiasa wanajua vema uhasiano wa Binti huyo na Mzee Ndejembi mkongwe wa siasa za chama tawala mkoani Dodoma .
Itakumbukwa ktk msiba huo alionekana Mzee Lowasa akiwa nyumbani kwao na Marehemu kutoa pole huku mwanasiasa mtata Zitto Kabwe akiandika ktk mitandao ya kijamii kutaka haki itendeke ktk kifo cha binti huyo.

NINI KILITOKEA KABLA YA MSIBA?
Taarifa za awali zinaonyesha marehemu Betty kabla ya umauti alisafiri nje ya nchi,baada ya kurejea hakwenda moja kwa moja nyumbani kwake bali alifikia kwa ndg yake akidai maumivu ya tumbo huku akionyesha matumaini ya kupona japo hakuwa akitumia dawa.

Muda wote akiwa hapo kwa ndg yake hakuweza kula chochote zaidi ya kunywa chai tu na alipofika jioni aliaga kwenda kwake mikocheni jambo lilipelekea kupewa mtu wa kumsindikiza hadi kwake.Usiku alilala vizuri japo kuwa tumbo lilikuwa bado likimsumbua.
Asubuhi ya kesho yake alipigiwa simu na mtu wake "kikazi" atoke nje wakutane wamalize mambo yao ,ombi alilokubali bila kujua kuwa alikuwa akienda kukutana na "israel" tangu muda huo hadi saa 10 jioni Betty alikuwa akipatikana kwenye simu yake na baada ya muda simu yake ilipotea hewani kabla ya asubuhi kupatikana akiwa hajitambui mtoloni. 
Ajabu na kweli hadi dk hii hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa kuhuisiana na kifo cha binti huyo aliyekuwa mhitimu wa chuo kikuu cha Dodoma.

Unataka kujua nini sababu ya kifo chake,ni mapenzi,dhuluma nk. na nani yupo nyuma ya tukio hilo asiyeweza kuguswa na mkono wa dola ? Ni mmoja wa mtoto wa Kigogo anayefadhili magenge ya wauza madawa ya kulevya hapa nchini jina kapuni kwa sasa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments