[wanabidii] NYERERE ALIJENGA HIVI , WENGINE WAMEJENGA NINI ?

Sunday, September 14, 2014
Tulipopata Uhuru tulijenga uchumi chochezi,Tumbaku ililimwa Tabora,Kiwanda cha Sigara kikatengenezwa Morogoro,Pamba ililimwa Mwanza na Shinyanga,Kiwanda cha nguo kikajengwa Mara,Dar es Salaam na Mwanza,Ng"ombe walifungwa Shinyanga,kiwanda cha maziwa kikajengwa Utegi Mara,lakini ili wasukuma wasikose vyote wakajengewa kiwanda cha Nyama mwaka 1974 ili kichochee ufugaji,katani ililimwa Tanga na Morogoro,kiwanda cha nyuzi kikajengwa Tabora,kwa sababu serikali ilitangaza kuwa kilimo ni uti wa mgongo,serikali ilijenga kiwanda cha dhana za kilImo mbeya,ilijua kabisa hii ni fursa,serikali ilijua kabisa lazima iangize magari kwa ajili ya shughuli za kiofisi na pia watu wake walikuwa wanaagiza magari,serikali ikaiona hii fursa ikajenga kiwanda cha matairi pale Arusha cha General Tyre,kwa sababu kipindi hicho hakukuwa na majiko ya umeme,mafuta wa gesi,wachumi waliojua watanzania tunatumia mkaa ama kuni,ikabidi serikali ijenge kiwanda cha kibiriti,kwa sababu kilimo kilikuwa kwa kasi,na ili utoe mazao shambani ulihitaji vifungashio,ilibidi kujenga kiwanda cha magunia kule Igowole.

Ili kupata wataalamu kila wizara ilijengewa chuo kwa ajili ya kutengeneza wataalamu mfano.
1.Wizara ya fedha....IFM na CHUO CHA UHASISBU DSM
2.Wizara ya Maji.......Chuo Cha maji Ubungo.
3.Serikali kuu..........IDM Mzumbe.
4.Serikali za Mitaa...Hombolo
5.Wasaidizi maofisini..Uhazili Tabora na Magogoni Dsm
6.Wizara ya Ardhi.....Chuo Cha Ardhi Tabora na Morogoro
7.Wizara ya Kilimo....Chuo cha Kilimo Nyegezi,Ukiriguru.
8.Ufugaji nyuki..........Chuo cha Nyuki Tabora.
9.Habari...................TSJ,sasa IJMC
10.Sheria...............Chuo cha mahakama lushoto.
11.Ushirika............Chuo cha ushirika Moshi.
12.Michezo.........Chuo cha Michezo cha Malya,
13.Elimu.............Vikajengwa vyo vya ualimu
14,Ili kupata wataalamu wa utafiti,vikajengwa vyuo vikuu ili watu wapate elimu ya shahada,ili eneo hilo hilo liwe na wataalamu upande wa watendaji,kukawa na vyuo maalum kwa ajili ya ngazi ya stashahada ya juu
n.k,kila sekta ilikuwa na vyuo mahususi kwa ajili ya kutengeneza wataalamu wa kisekta.

Ili viongozi wajue maana ya uongozi,walijengewa maeneo ya kupumzika maarufu kama Leaders club.

Wizara zote zilijengewa miundombinu,mashule yote yalikuwa na nyumba za wafanyakazi,mabenki yakajengewa maghorofa kila mkoa pamoja na miundombinu mingine,shirika la reli likajengewa miundo mbinu kila mkoa,maghorofa,mahotel makubwa na clubs,Miundombinu hii haikujengwa kwa bahati mbaya,bali ilijengwa ili kuifanya kila wizara ama sekta inapoyumba ikopesheke,ndiyo maana wengine tulishangaa inakuwaje NBC ifilisike na kuuzwa kwa bei ya mandazi?,kwa kujidai tunajua sana,tuliuza kila kitu na kutupilia mbali kila kitu,matokeo yake sasa tumegeuka kuwa wachuuzi,hatuna uwezo hata wa kutengeneza nguo za ndani wala njiti za vibiriti,tumeamua kuwa taifa la kichuuzi,kama miaka ya 70 tuliweza kuwa na kiwanda cha magari,nini kinatushinda leo?mbona maprofesa na wasomi ni wengi lakini tunatengeneza taifa la kichuuzi?NAWAZA TU WANAJAMVI.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments