[wanabidii] Mapendekezo ya Kamati za BMK kuhusu mgawanyo wa madaraka, Mahakama ya Kadhi, Uraia, Haki za Wanaume

Friday, August 22, 2014
Kamati namba 1 na 11 za Bunge Maalumu la Katiba zimetaka Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Mkuu kuwa Makamu wa pili.

"Makamu wa kwanza awe ni Rais wa Zanzibar na wa pili awe ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ili kumpa mamlaka Rais wa Zanzibar…kwenye kamati yetu tumeondoa neno nchi washirika na Waziri Mwandamizi," amenukuliwa akisema Mwenyekiti wa kamati namba moja, Ummy Mwalimu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati namba 11, Hamad Yusuph Masauni, alisema kamati yake imependekeza kuwa na Makamu wa Rais ambaye ni Rais wa Zanzibar ili kumwezesha kutambulika nje ya nchi kama 
Makamu wa Rais wa Tanzania.

Pia, Masauni alisema kamati yake imependekeza uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya uwe na uthibitisho wa Bunge ili kuondoa kuteuliwa watu wasio na sifa na urafiki.

Mwalimu alisema mambo matatu yamekosa theluthi mbili na kwamba yatapelekwa kwenye Bunge Maalum kwa ajili ya umuzi zaidi. Aliyataja kuwa ni Mahakama ya Kadhi, Uraia Pacha na Haki za wanaume.

Aidha, alisema masuala ya ndoa, imani, mirathi na takala yameachwa kwa dini husika na kwamba serikali haitahusika na masuala ya kidini. 

NIPASHE - Mgawanyo wa madaraka ya Serikali moto Bunge la Katiba

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments