[wanabidii] KAMA ULIKATALIWA NA NYERERE HUTUFAI

Sunday, August 24, 2014

Hakuna aliyewahi kukataliwa na Mwl.Nyerere akafanikawa na Mzee alikuwa hamkatai mtu bila ya sababu..

Nawaambia vijana wenzangu popote... We must get up and stand up for our nation!!!

Kuna madalali wanapata pesa nyingi kwa ajili ya kutuingizia kiongozi wa watanzania.

Kuna walio na matarajio yao wanayajua wenyewe.

Wanawadanganya vijana watawapa pesa za kugombea ubunge kumbe hakuna atakayepewa hata shilingi, sanaa tu za kutafuta kura.. Huku wakiwatumainisha vijana mgombea wao ni lazima ashinde ili wapate Moyo wa mapambano.

Amkeni.. Hayo ndio mabadiliko ya kifikra.

Hili ni taifa... Haliwezi kupatikana kwa nguvu ya pesa wala uongo.. Bali mkono wa mungu utachukua nafasi yake.

Mwl alisema " muogopeni sana mtu anayetafuta cheo kwa nguvu huku akitumia fedha' huyo kamwe hatatufikisha.

Ni jukumu la kila mwanaCCM kupeleka the right candidate kwa watz mil50.

Baada ya hapo kila mtu akatafute shamba alime.. Apate chakula cha watoto wake.

Huwezi kusema unataka kuwa mwanasiasa wakati hauna mapenzi ya dhati na taifa lako. Ni kutafuta vyeo tu..

Sifa kubwa ya mwanasiasa bora huwa halipi Fadhila... Unaweza ukasaidiwa kwenye kampeni. Lkn mtu kama hafai unamwambia hufai tu..

Siasa za kulipana fadhila ni ujinga kabisa...

Huwez kuwa mwanasiasa kama unawaza vyeo tu.. Na kutoka kimaisha huwezi...

Kwsbb hautaweza kusema kweli. Utakuwa mtu wa kujipendekeza tu ndani ya nchi yako na kuwa mwoga.

Mnaogopa kikwatwa majina.. Sijui kukosa vyeo ni ujinga mtupu.

Sikuzote siasa ni ww mwenyewe..

Ukatwe jina, ukose cheo, siasa ipo palepale utaifanya tu.. Tena huku ukipanda daladala na kula kwa mama ntilie

Siasa ni wito wa kitume kuwatumikia watu.. Siasa sio madaraka

Mwl alisema kw mtu muadilifu kabisa ikulu ni mzigo.. Kuna watu wenye shida na matatizo mbalimbali wote wanakuangalia wewe.

Watu wajinga wanawaza nimsaidie Fulani akiingia ikulu na sisi tupate hiki na kile... Sasa utajiita mwanasiasa au tapeli?

Ile dhana ya wito wa kitume hauna unatafuta maisha tu... Sio utume.

Ni Heri useme ukweli kwamba kiongoz sahihi kwa watanzania ni huyu hatakama akikosa..

Hakuna kuogopa kwamba ikitokea ninayempinga ndio kapata itakuwaje? Huo ni ujinga na hiyo sio siasa...

Politics ni unapiga zege unalipwa ujira wako unakwenda kufanya siasa....

Ukianza kuwaza fedha na Mali hauwez kuwa mkweli..

Mali na fedha unatafuta mwenyewe pending. Out of politics.

Naonaga watu wanaandika. Hawapambani kwa ajili ya kuondoka utumwani ila wanapambana ili waje kuwa mabwana!

Mungu wangu.

Mi nilifikiri tunafight kwa ajili ya watanzania kumbe shida yetu ni ubwana!?

Hakuna mtumwa Tanzania.. Ila hii ni nchi na ina taratibu zake.

Wito wangu.

Kama mtu anasema anataka kufanya siasa basi na ajikane nafsi yake.

Tupo kwa ajili ya wito wa kitume.. Kuwatumikia watanzania wenzetu ambao kuna wengine jana wamelala bila ya kula.

Sisi tumekulia maisha ya kulala na njaa.. Tunajua tabu za watu that's why hatupend masihala.

Itasambazwa social networks zote..

Tutaeleweshana taratibu. Tutabadilika na tutakuwa sahihi kwa manufaa ya taifa .


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments