[wanabidii] Wajumbe wa Tume hulipwa Kiasi gani cha fedha nchini Tanzania

Monday, February 25, 2013
Habari wadau,
Napenda kufahamu ni kiasi gani wajumbe wa tume hulipwa pale wanapoteuliwa kutekeleza majukumu yao.
Na wajumbe hao, hilipwa kwa siku au kwa mwezi?
Wajumbe hao hukipwa mishahara au posho?
Ni lini bajeti ya tume ilitengwa na kuidhinishwa na kikao gani ili fedha hizo zitumike?
Ni kwa nini sisi walipa kodi mara nyingi hatudai matokeo ya tume ili kujua fedha yetu inatumikaje?
Hivi karibuni waziri mkuu Pinda ameunda tume kuchunguza sababu za kufeli mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Naomba kujuzwa kwa wale mnaofahamu mambo haya yakoje.
 
Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 

Share this :

Related Posts

0 Comments