[Mabadiliko] KUTOKA CHADEMA KUELEKEA ACT, NI KUHAMA AU KUKIMBIA?

Saturday, August 30, 2014
Ninashangazwa sana na hii kasi ya kuhama Chadema Kuelekea ACT kwa mujibu wa taarifa nyingi kwenye media, sina uhakika sana kama Chadema ni mbovu kiasi cha kuwanyima wanachama uhuru wa kutoa hoja na kuelezea yale yanayopaswa kufahamika kwa faida ya wananchi.

Chadema ni chama cha watanzania, au kundi fulani la watu ambao wamejijengea ka-Kingdom kiasi kwamba wao ndio Alfa na Omega na asiyetaka aondoke? Kwa nini sasa na si wakati mwingineo?

Huko ACT ndiko kweli kwenye fursa ya kila mtu kuongea bila hofu na woga tofauti na inavyoonekana ndani ya Chadema, ambako hadi Bwana MKubwa fulani akukubali ndio kieleweke?

Nawaza tu lakini nahitaji majibu. Isije kuwa hata huko ACT kila mtu huko akataka kuwa Mwenyekiti, ama Katibu ama BOSI kwani pia panatakiwa nidhamu kama mnataka ridhaa ya Wananchi. Huko pasigeuke garbage ya kila mtu kwenda tu kumaliza njaa au hasira zake simply because hakupata pa kupumlia ndani ya Chadema.

Tunahitaji pia kuangalia rekodi za watu ambao kazi yao imekuwa ni kuhama toka chama kimoja kwenda kingine, hawa wanasukumwa na nini? Wao ndio wanaonewa kila mahali?

Nashangaa eti hata UKAWA baadhi wamekuwa wakiomba iwe  Chama cha Siasa tofauti kabisa na lengo la awali lililopelekea kuundwa kwake. Kuna watu wengi ni wavivu wa kufikiri ila ukianzisha jambo wao wanalibeba bila kutafakari na kuzunguka nalo kila pahali na kulifanya "temporarily" topic of a day!

Kuhamahama na kubadili vyama kila siku ndio uzalendo wa kweli? Sisi wananchi wa kawaida tunaowasikilizeni ninyi tujifunze nini na tuamini lipi kama mnabadilika badilika kila baada ya muda? Sio Njaa kweli hii? Tutafika kwa mtindo huu kisiasa? Hamuwezi kusimamia hizo haki zenu ndani ya Chadema hadi mkimbie? What  if hata huko ACT pakigeuka in future, will you again run away? For how long will you keep running here and there?

Ndio nyinyi mwakani mnatarajia kuomba uwakilishi majimboni kwenu kwa utaratibu huu? Labda hao raia ni vipofu na hawawezi kufikiri.

Hebu tuwape mwaka mmoja hawa wote wanaokimbia vyama vyao tuone watakuwa wapi kitakwimu kuelekea uchaguzi ujao.

Dawa ya tatizo ni kukimbia tatizo ama kukabiliana na tatizo? Kama umma uko nyuma yako unakimbia nini? Si usimamie hapo hapo ulipo?

Field Marshal Mwagika, unahitajika kutoa somo la Team Building na phases zake na problems associated kwa hawa ndugu zetu..Wanakosa uzoefu na Uvumilivu wa kisiasa. Hizi ni ups and downs ambazo haziepukiki kama tumedetermine kuleta mabadiliko ya kweli, wa kuumia wapo lakini mwisho wa siku ni katika harakati za kuijenga nchi. There is no easy / smooth transition katika kujenga demokrasia, kukimbia ni kuwaumiza wananchi ambao wako nyuma yao, ni kondoo wanaoachwa bila mchungaji. Hiyo Imani mtapewa na nani huko ACT? Ni hawa hawa  mnaowakimbia sasa. 

Kuna kiongozi ambaye amefanya mikutano na wananchi wake na kuwaeleza nia ya kuondoka na sababu za msingi na wakabariki kuhama kwake ama wanasikia tu breaking news kwenye media kama mimi?


Stop & Think before making any impacting decision! See it in a big picture, not individually.

Omukunirwa Ireneus 


 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAN5khk4ORAaKG5cegEesLdZHH6JMKACEvZCiyEjVyny8fHhtJQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments