Naishangaa serikali na vyombo vyake vya dola hasa jeshi la polisi. Iweje wafanye mauaji ya kutisha na serikali isitoe tamko kwa waliohusika. Wao wakikamata kibaka wanampiga na kumburuza mahakamani hadharani, lakini wao wakiua raia wanapelekwa mahakamani wakiwa wamefunikwa kama wanawali. Bandugu mnalionaje hili?
Walomuua Generali Kombe wako mtaani,
Walomuua Mwandishi wa habari iringa wako mtaani,
Walomtesa Dr. Ulimboka, wako mtaani;
Walotaka kumuua Highness na Mbunge wa Ukerewe, wako mtaani,
Kwa ujumla jeshi hili limekosa sifa za kuitwa la usalama wa raia na mali zao badala yake ni kinyume.
Wewe Mwanabidii unalisemaje hili?
Mt. B;
Bukoba Municipal,
Bukoba Municipal,
Tanzania - East Africa.
0 Comments