Vipaumbele vyake
Makamba alibainisha vipaumbele vyake endapo atateuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo kuwa ni pamoja na kushughulikia tatizo la ajira, huduma za jamii, uchumi imara na utawala bora.
Akifafanua vipaumbele hivyo alisema, watu wamekuwa wakizungumzia suala la kutatua tatizo la ajira kwa wembamba na sio kwa mapana, lakini yote haya yanatokana na kipato chao kuwa chini.
"Mazingira katika uchumi bado siyo mazuri, nitahakikisha kila mtu mwenye kipato cha chini anakuwa na kipato cha kati na mwenye kipato cha kati anakuwa na kipato cha juu kwa hali hii vijana wetu hawatakimbilia kuajiriwa, bali watataka kujiajiri wao kwani watakuwa na mitaji kutoka katika vipato vyao," alisema.
"Kuhusu huduma za jamii kama elimu, afya na maji... na zenyewe yapo mawazo ya kuboresha kwani huwezi kuendesha taifa lisilokuwa na huduma nzuri kwa wananchi."
Kuhusu suala la uchumi alisema, utaimarika endapo huduma za umeme, usafirishaji na mawasiliano zitaimarika kwani zitawasaidia wananchi kufanya shughuli zao kikamilifu.
"Huwezi kuongoza nchi kama utawala bora haupo. Hapa tutaangalia namna ambavyo tutaendesha Serikali... namna ambavyo haki zinatolewa kwa wananchi kwa wakati," alisema Makamba.
Aliongeza: "Haya ndio mambo ambayo nimeyawaza na kuona kama changamoto kwangu. Nitakayafanyia kazi kuona Tanzania, kama ni katika ngumi, katika uongozi wangu (Tanzania) iwe inapigana katika uzito wa juu kabisa."
Awamu ya vijana
Katika mahojiano hayo, Makamba alisema umefika wakati vijana wakashika dola kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza katika awamu nne za utawala wa chama chake cha CCM.
Alisema marais wote wanne, Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete wamefanya kazi nzuri na kuitambulisha nchi kimataifa, hivyo zinahitajika fikra mpya kuendeleza raslimali nyingi zilizopo.
Kuhusu uzoefu wake
Akizungumzia uzoefu, Makamba alisema hakuna ushahidi wowote kwamba miaka mingi kwenye siasa ndiyo inatengeneza kiongozi mzuri.
"Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira, uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa. Sifa hizi hazipatikani kutokana na uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo," alisema.
Alitoa mifano mingi duniani ambako vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
"(Rais wa Marekani,) Barack Obama alikuwa seneta kwa miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na umri miaka 39 tu," alisema Makamba. "Kama sasa hivi tuna malalamiko mengi kuhusu jinsi mambo yanavyokwenda, je, tunahitaji kiongozi ambaye kwa miaka 30 amekuwa sehemu ya mfumo tunaoulalamikia? Jibu ni hapana."
Je, CCM ipo tayari kuwaachia vijana? Akijibu swali hilo, Makamba alisema chama hicho kipo tayari na kimeshatoa fursa kwa vijana kushika nyadhifa za uongozi wa juu, akiwamo yeye.
"Chama chetu (CCM) kinasikiliza umma wa Watanzania na mahitaji yao. Umma wa Watanzania unahitaji mabadiliko makubwa na CCM itaongoza mabadiliko hayo kwa kulipatia Taifa hili uongozi mpya wa kizazi kipya," alisema Makamba.
Akizungumzia uwezekano wa chama hicho kuamua kutoa fursa hiyo ya juu kwa mwanamke, Makamba alijibu, "Kila mtu anaruhusiwa kugombea."
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/January--Nagombea-urais-2015-kutekeleza-vipaumbele-vinne/-/1597296/2371534/-/item/3/-/14c8waqz/-/index.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments