[wanabidii] Tahadhari ya Bodi ya Mikopo kuhusu utapeli kwa waomba mikopo ya Elimu

Friday, July 04, 2014
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

Plot No. 8, Block No. 46, Sam Nujoma Road, Mwenge; P.O. Box 76068, Dar es Salaam, Tanzania

Tel: (General) +255 22 2772432/2772433; Fax: +255 22 2700286; E-mail: info@heslb.go.tzWebsite:www.heslb.go.tz

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwatahadharisha waombaji wa mikopo na umma kwa ujumla, juu ya kuibuka kwa genge la matapeli wanaowalaghai wananchi ambapo hujitambulisha kuwa wao ni wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo.

Mbinu zinazotumiwa na genge hilo la matapeli ni kuwatumia ujumbe mfupi wa simu waombaji wa mikopo ukiwatahadharisha kuwa fomu zao za maombi ya mikopo zina dosari na hivyo wanatakiwa watume sh. 15,000.00 kwa kutumia utaratibu wa kutuma Fedha kwa njia ya mitandao ya simu kwenda kwenye namba za simu za matapeli hao ili fomu zao za mikopo ziweze kufikiriwa.

Katika utapeli huo, matapeli hao wanawatishia waombaji wa Mikopo wanaoendelea na masomo kuwa wasipohuisha taarifa zao za kuendelea kupokea Mikopo mwaka ujao wa kitaaluma 2014/2015 hawatapata Mikopo.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwafahamisha waombaji wa Mikopo na umma kwa ujumla kwamba:

(i) Waombaji mikopo wanatakiwa kutuma fomu zao au taarifa zilizokosekana kwa njia ya Posta tu. Bodi haijaweka wakala mwingine yeyote anayetoza ada kwa ajili hiyo.

(ii) Ada zote za maombi ya mikopo zilielekezwa kulipwa kwa njia ya M-Pesa kwa utaratibu ambao umeelekezwa bayana kwenye ukurasa wa maombi kwa njia ya mtandao (http://olas.heslb.go.tz) na si vinginevyo.

(iii) Waombaji wa Mikopo wanaoendelea na masomo hawatakiwi kujaza fomu za maombi ya Mikopo kama ilivyokwisha kufafanuliwa katika Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

(iv) Waombaji mikopo watakaopokea simu au ujumbe mfupi wa simu unaowataka watume Fedha ili wapatiwe huduma ya kuhuisha taarifa zao za mkopo watoe taarifa kuhusu matapeli hao kwa Polisi au TAKUKURU kusudi hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahalifu hao.

IMETOLEWA NA:

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments