Namshukuru Mbunge wa Mwibara kwa ushujaa wa kuweza kutamka wazi kuwa serikali ya CCM inaendeshwa kisanii. Kibaya zaidi mpaka Jeshi la Polisi nalo linaendeshwa kisanii ndo maana waliweza kumbambikia chizi kesi ya kumjeruhi Dr Ulimboka!
Kinachotisha mpaka uongozi wa jiji la Dar es salaam nao wanaendesha usanii wa kusafisha jiji kwa kuwabeba Wamachinga na bidhaa zao kwenye malori ambayo yangeweza kutumika kuzoa takataka zilizojaa kila kona ya Dar es salaam. Mfano mzuri ni lundo la takataka lililojaa pembezoni mwa ukuta wa Shule ya Jangwani pale Faya ambalo lina zaidi mwezi bila kuzolewa.
Jiji hao hao waliendesha usanii wa kuvunja paa za nyumba za watu na kuleta uharibifu wa kutisha kwa kisingizio cha kusafisha jiji la Dar es salaam wakati Jiji nini chafu kiasi cha kutisha.
Tumwombe Mwenyezi Mungu atuondolee usanii huu wa kutisha kwenye nchi yetu.
0 Comments