1) Mashindano ya Ligi iliyodhamniwa na mtu aitwaye Bashiri, imeahirishwa baada ya jogoo aliyekuwa atolewe kama zawadi, kuibiwa.
Kutokana na tukio hilo, michezo imeahirishwa, huku waratibu wakihaha kutafuta hela ya kununua kilo tano (5) za dagaa kama mbadala wa jogoo. Hawajazipata!
2) Ligi nyingine imesimama baada ya washiriki kugomea "zawadi" ya mchele aina ya kitumbo. Waratibu wa ligi hii ya pili,nao wanajitahidi kupata Tshs.10,000/=, ambayo ni tofauti ya bei ya mchele wa kitumbo kilo 5 na ule wa super.
Chanzo: Gazeti la Jamhuri la Jumanne.
Kwa bahati mbaya haikuelezwa mashindano hayo yanafanyika wapi.
Binafsi, baada ya kusoma habari hii, nilipata shauku za aina mbili:
Kwanza, niliangalia jinsi tunavyoweza kuendeleza tasnia ya michezo katika mazingira haya. Nikaona "mfadhili" huyu anafanya kazi miongoni mwa watu wenye hitaji hili la chakula.Lakini nikajiuliza, kwenye ligi kama hii, mchezaji kama huyu akiumia, atahudumiwa vipi, au ndio kuwa kilema?
Pili, je jitihada za "wadhamini" kama hawa, ikizingatiwa kuwa wana wa engage vijana wasio na ajira, hivyo kuwa "keep busy wasishiriki kwenye matendo maovu, tunahitaji kuziunga mkono? Kwa kiasi gani? Au tuwazuie? Labda wanataka kuja "kugombea"
Tutafakari.
MJL
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments