[wanabidii] R I P USTADH ILUNGA

Monday, May 05, 2014

INNA LLILAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN

Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za msiba wa kufariki Ustadh Ilunga. Kifo kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Ustadh Ilunga amefanya mengi ya muhanga katika Uislamu hususan kuwaamsha Waislamu juu ya dhulma kubwa ya ubaguzi na kupendelewa Wakiristo katika serikali ya Tanzania katika miamala mbali mbali.

Taaarifa za awali tulizozipokea zinasema marehemu ataswaliwa Msikiti wa Kichangani Magomeni jijini Dar-es Salaam. Tunawaomba mashababu wote wa hizb jijini Dar(haswa) na Waislamu wote (amma) tushiriki kikamilifu kumswalia ndugu yetu na kushiriki kikamilifu katika maziko yake.

Kwa niaba ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki tunatanguliza mkono wa dhati wa taazia kwa Waislamu wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Ustadh wetu Ilunga.

Tunamuomba Allah SW kwa utukufu wake Awape wafiwa ujira mkubwa, Amsamehe ndugu yetu huyu, amjazie penye mapungufu na Amuingize katika pepo yake ya daraja ya juu- Ameen

Masoud Msellem

Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari - Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments