Katika Bunge la katiba leo nimemsikia WAziri Mkuu akisema kuwa Kama mawaziri hawatakuwa wabunge hawataweza kuwa karibu na wananchi. Anafafanua kuwa hawataweza kuyajua matatizo wananchi wanayokabiliwa nayo.
Kama nimemuelewa ngoja nifafanue:
kwamba Mbunge wa Jimbo la Muleba magharibi ambaye anayaelewa matatizo ya wanajimbo lake akichaguliwa kuwa waziri wa Afya atakuwa anayaelewa matatizo ya watanzania kutoka majimbo zaidi ya 300 kwa kutembelea jimbo lake.
Jingine nililolielewa ni kwamba kama Mtanzania anayeishi Misungwi akichaguliwa kuwa waziri wa Afya hataweza kuyaelewa matatizo ya watanzania yahusuyo afya kwa sababu hana jimbo analotembelea.
naendelea kufafanua. Waziri Mkuu anaamini kuwa waziri wa afya hategemei faarifa za idara yake kutoka mikoani na kutembelea maeneo husika baada ya kusoma taarifa hizo ila mpaka awe mbunge.
Sipendi kuendelea kujadili zaidi ya hapo kwa sababu naamini hakuna ambaye hawezi kuelewa namna Waziri asiye mbunge anavyoweza kuwajua watanzania na tena jinsi ubunge usivyomsaidia wwaziri kuijua tanzania na matatizo yake.
Ninaweza tu kuongeza kuwa wapo wamisionari wanayaelewa na kuyaeleza matatizo ya watanzania kuliko wabunge wetu. Huwa wawasikia wabunge wetu wakiwauliza mawaziri matatizo yaliyoko majimboni mwao na mawaziri huyajibu sawasawa na wabunge wakajua hali hizo kutoka kwa mawaziri wanaokuwa hawaishi kwenye jimbo la mbunge huyo. majibu hayo mawaziri huyapata kutoka kwa idara zao husika zinazopatikana mikoani na wilayani.
Lakini najiuliza swali moja INAKUWAJE WAZIRI MKUU HAJUI HILI?????
Elisa Muhingo
0 Comments