[wanabidii] MAJIBU/MAELEZO YA PINGAMIZI LILILOWEKWA NA MGOMBEA WA CUF CHALINZE DHIDI YA CHADEMA

Friday, March 14, 2014

MAJIBU/MAELEZO YA PINGAMIZI LILILOWEKWA NA BWANA FABIAN L.SKAUKI DHIDI YANGU MIMI MATAYO M.TORONGEY MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA). UTANGULIZI . Kwa mujibu wa ibara ya 67 (1) ya Katiba ya Jamhuri Muungano wa Tanzania (1977) inaeleza wazi kuwa ili mtu ateuliwe kuwa mgombea ubunge ni lazima awe na sifa zifuatazo; 

(i) Awe raia wa Tanzania 

(ii) Awe ametimiza umri wa miaka ishirini na moja 

(iii) Awe anajua kusoma na kuandika kwa Kiswahili au Kiingereza

 (iv) Awe ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa

 (v) Awe hajatiwa hatiani na mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kodi yoyote ya Serikali katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi. Aidha, Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (2) na (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977; hata kama mtu ana sifa zote za kugombea hataruhusiwa kugombea Ubunge kama : 

(i) Ni raia wa nchi nyingine; au (ii) Kwa mujibu wa Sheria iliyotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au

 (iii) Amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda usiozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au 

(iv) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa Umma; au

 (v) Siyo mwanachama na siyo Mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa; au 

(vi) Ikiwa mtu huyo ana maslahi yoyote katika mikataba na serikali ya Jamhuri ya Muungano au serikali ya mapinduzi Zanzibar wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalumu kwa mujibu washeria iliyotungwa na Bunge, na iwapo amekiuka miiko hiyo; au

 (vii) Ameshika madaraka ya Afisa Mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais anaweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, au sheria iliyotungwa na Bunge; au 

(viii) Kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kuandikishwa kama Mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge. 

(ix) Ni mgombea Urais /Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, kwa mujibu wa masharti kwa vyama vya siasa na wagombea uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kifungu cha 5.3 kimeweka masharti ya Uteuzi wa Mgombea Ubunge na kuweka kama ifuatavyo; 

(i) Awe amedhaminiwa na wapiga kura wasiopungua ishirini na tano waliojiandikisha kupiga kura katika Jimbo hilo. 

(ii) Mgombea haruhusiwi kujidhamini yeye mwenyewe 

(iii) Awe na dhamana ya shilingi 50,000/= 

(iv) Awe ametoa tamko la kisheria mbele ya hakimu kwamba anazo sifa zinazotakiwa ili kugombea Ubunge Vilevile, kwa mujibu wa masharti kwa vyama vya siasa na wagombea uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kifungu cha 6.0 kimeweka utaratibu wa Pingamizi dhidi ya uteuzi wa Mgombea Ubunge: Na Kifungu cha 6.3, kimeweka sababu za kuweka Pingamizi kuwa ni:

 (i) Maelezo yaliyopo katika fomu ya uteuzi hayatoshi kumtambulisha Mgombea;

 (ii) Fomu ya Uteuzi haitimizi au haikuwasilishwa kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sharia; 

(iii) Kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika fomu ya uteuzi ni dhahiri kwamba Mgombea uchaguzi hana sifa zinazotakiwa; 

(iv) Uthibitisho wa Msimamizi wa Uchaguzi unaopaswa kutolewa haukutolewa; (v) Mgombea hana sifa zote zinazotakiwa; 

(vi) Hakuna uthibitisho kuwa Mgombea amelipa dhamana ya shilingi elfu hamsini (50,000/=); na (vii) Hakuna picha ya Mgombea. 

(viii) Mgombea hakujaza fomu Na.10 kuthibisha kuwa ataheshimu na kutekeleza maadili ya Uchaguzi. Baada ya utangulizi huo hapo juu ambao unaonyesha dhahiri kuwa hapakuwa na sababu yoyote ya mimi kuwekewa pingamizi na Mgombea ubunge wa Chama cha CUF, kwani hakufuata masharti ya Katiba, Sheria na maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kwetu kama wagombea, kwani aliamua kutunga mambo ambayo yapo nje ya utaratibu na hayakidhi haja, hayakufuata Katiba, matakwa ya kisheria na hata maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 

Nayasema yote haya kutokana na ukweli kuwa mimi nimekidhi sifa zote za kuwa Mgombea Ubunge na nimetimiza masharti yote yaliyowekwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kutokana na barua yako ya tarehe 13 Machi, 2014 yenye kumbukumbu namba HWB/E.50/21/76 nalazimika kujibu pingamizi hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya Uchaguzi sura Na.343 kifungu Na.40 (5) kuhusu pingamizi, hata kama halina nguvu kwa mujibu wa katiba, sheria na maelekezo ya Tume ya taifa ya uchaguzi hoja kwa hoja kama ifuatayvo. 

MAJIBU YA HOJA ZA PINGAMIZI LA FABIAN LEONARD SKAUKI:

 1. HOJA YA KWANZA; Kwamba mimi Mathayo Mang'unda Torongey nimejaza taarifa za uongo kwenye fomu zangu kuwa kazi ninayoifanya ni BIASHARA na kusema kuwa ni taarifa za uongo kwa kuwa sikuweka vielelezo vya kuonyesha kuwa mimi ninafanya kazi hiyo, na kuwa sijulikani ninafanya kazi gani .

MAJIBU YA HOJA YA KWANZA : Pingamizi na sababu zilizotolewa na Mgombea wa chama cha wananchi CUF Bwana Fabian L.Skauki hazina mashiko na kuwa yeye ameamua kukupotosha kuwa mimi sio mfanyabiashara kwa kuwa sikuweka vielelezo, japo ni wazi kuwa sikupaswa kuweka vielelezo vyovyote kwani fomu haikuwa inanitaka kuweka vielelezo vya aina yoyote kama ambavyo hata yeye hakuweka vielelezo kuwa anafanya shughuli gani. 

Ninasikitika kuwa hata wewe Msimamizi umekubaliana na hoja hii dhaifu ya pingamizi na kunitaka mimi kuijibu wakati unajua wazi kuwa haina mshiko wala mantiki kwa mujibu wa sheria za uchaguzi. Naambatanisha leseni yangu ya Biashara yenye jina langu namba B.No. 01299270 iliyotolewa tarehe 19/09/2011 na huo ni uthibitisho kuwa mimi ni mfanya biashara (kielelezo A) 

2. HOJA YA PILI: Kwamba, mimi Mathayo Torongey sijui kusoma wala kuandika Kiswahili au Kiingereza, na kwamba nimedanganya na hivyo sina sifa za kuwa Mgombea Ubunge. 

MAJIBU YA HOJA YA PILI; Kwanza, nieleze wazi kuwa nimesikitishwa sana na tuhuma hizi ambazo zina lengo la kunichafua mbele ya jamii na Taifa kwa ujumla, zina lengo la kuichafua jamii ya watanzania kutoka familia za wakulima na wafugaji, watu ambao wana kipato kidogo na ambao wanaishi vijijini kuwa ni watu wa hovyo na hawajui kusoma wala kuandika, ni tuhuma za kuwadhalilisha watanzania ambao ni kutoka jamii za wananchi wa vijijini wanaotafuta fursa ya kuchaguliwa kwamba ni watu wa wanaoomba nafasi wakiwa hawajui kusoma wala kuandika, kwa kweli nasikitika sana kwa hili na lilikuwa tusi ambalo msimamizi wa uchaguzi hukupaswa kulipokea. Aidha, nashindwa kutoa ushahidi hapa kwani hata wewe umeziamini tuhuma hizi kuwa mimi sijui kusoma wala kuandika na ndio maana ukanitaka nizijibu, japo ni ukweli ulio wazi kuwa sahihi yangu kwenye fomu haikuwa ya "kuweka dole gumba" niliweka sahihi kwa kuandika na mbele yako na sikuandikiwa. Pili; Yafaa mgombea huyu pamoja na wale wote waliomtuma wakatoa ushahidi wake kwako kuwa mimi Mathayo Mang'unda Torongey sijui kusoma wala kuandika, na hii itamsaidia kuaminika mbele ya jamii ya wananchi wa Chalinze ambao anataka kuwaongoza. Hata hivyo naomba nitoe majibu mbele yako kwa maandishi na kwa kusoma kitu ambacho wewe utataka nisome na kuandika ili uwe uthibitisho kwako kuwa najua kusoma na kuandika . 

3. HOJA YA TATU: Kwamba, mimi Mathayo Torongey nimedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini walionidhamini kuwa Mgombea na kuwa sahihi zote zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kuwa sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio mhusika . 

MAJIBU YA HOJA YA TATU: Kwanza, nieleze wazi kuwa nilipokamilisha kujaza fomu zangu na kudhaminiwa na wadhamini 25 kwa mujibu wa sheria , nilikuja ofisini kwako na tukakagua kwa pamoja majina ya wadhamini wote waliokuwepo kwenye fomu zangu na nilikuja na shahada zote za wapiga kura ambao walinidhamini na wewe ulizikagua na kuridhika kuwa walikuwa ni wapiga kura sahihi na saini zao zilikuwa sahihi na uliandika hilo kama uthibitisho wako kwenye fomu zangu za uteuzi na ndio maana uliniteua kuwa mgombea . Pili, Namshangaa mweka Pingamizi kwa kuja na tuhuma kuwa saini za wapiga kura zinatofautiana na saini zilizoko kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura ,hii ni kutokana na ukweli kuwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura hakuna saini za wapiga kura isipokuwa saini zipo kwenye vitambulisho vya wapiga kura, na vitambulisho hivyo niliviwasilisha kwako na wewe kama msimamizi wa uchaguzi baada ya kukagua vitambulisho hivyo uliridhika kuwa saini za wadhamini wangu zilikuwa sahihi na ndio maana uliniteua kuwa Mgombea na kuweka "uthibitisho wako" katika kifungu F. kwa maandishi kwenye fomu zangu za uteuzi. Naomba kunu

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments