Niko na DVD player, jana jioni na leo asubuhi nimetembelea vijiwe vya kahawa vitatu,,,huko kwa pamoja tuliangalia DVD yenye hotuba za mh.Zitto Kabwe. Jamani siasa za kwenye mtandao tafauti kabisa na za kitaa, watu ni waelewa kweli.
Mzee mmoja kwa kutumia lugha ya kihehe alisema mtu kama Zitto zamani tuliwaona kama miungu na sasa waweza kumuona kama Nabii. Mimi nikamwambia, Zitto si nabii na wala hafanani na mungu hata nukta moja. Nikaendelea kumwambia, tafauti kati ya Zitto na wanasiasa wengi wa nchi yetu ni kuwa Zitto ni mzalendo na anauchungu wa nchi wakati wengine ni wahafidhina na wanauchungu na mitandao yao ya kifisadi. Mzee akanielewa na akaendelea kusema
"basi anafaa kuwa rais"
"tatizo umri na tuvute subira" nikamjibu
Niseme tu, humu mtandaoni mtapata mrejesho tu lakini siasa tutapiga kitaa, sasa tutapiga Mkoa kwa mkoa,,nyumba kwa nyumba, vyovyote iwavyo, kama tunauhibiri uzalendo au tunaufundisha, lakini tunataka watu wawe wazalendo, hata titi la mama tulijifunza kunyonya, ndio sembuse uzalendo?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments