[wanabidii] Uteuzi wa makatibu tawala , kuwahamisha wengine na wakurugenzi wa majiji

Sunday, January 19, 2014
Rais Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa mitano na kuwahamisha makatibu tawala wengine na wakurugenzi wa majiji.

Makatibu tawala wapya ni ndugu Wamoja A.Dickolangwa anayeenda mkowa wa Iringa ambako alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa,ndugu Abdallah D.Chikota anayeenda Lindi kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Newala,ndugu Symthies E.Pangisa anayeenda mkoa wa Rukwa kabla alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara,ndugu Alfred C.Luanda aliyeteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa Mtwara kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora,ndugu Jackson L.Saitabau anakwenda mkoa wa Njombe kabla alikuwa katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Arusha.

Waliohamishwa ni Beatha Swai kutoka katibu tawala mkoa wa Pwani kwenda ofisi ya waziri mkuu,TAMISEMI,ndugu Sipora J.Liana,kutoka mkurugenzi wa jiji la Arusha kwenda ofisi ya waziri mkuu,TAMISEMI,ndugu Benedict ole Kuyan kutoka katibu tawala mkoa wa Tanga kwenda katibu tawala mkoa wa Mara,ndugu Salum M.Chima kutoka katibu tawala Rukwa kwenda Tanga na Ndugu Mgeni Baruani kutoka katibu tawala mkoa wa Njombe kwenda katibu tawala mkoa wa Pwani.

Wengine ni Ndugu Juma R. Idd kutoka mkurugenzi wa jiji la Mbeya na kuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha,Eng.Omar Chambo aliyekuwa katibu mkuu wizara ya uchukuzi amehamishiwa mkoa wa Manyara kama katibu tawala wa mkoa,Dkt John Ndunguru aliyekuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi anahamishiwa mkoa wa Kigoma kama katibu tawala wa mkoa huo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments