[wanabidii] JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND KUSUMBUA TENA ULAYA,

Monday, July 04, 2016






Na Zainab Ally Hamis
Dar es salaam School of Journalism(DSJ)

Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea majukwaa ya maonyesho Afrika-Karibik, siku ya jumamosi 16 Julai 2016 mjini Bayreuth,Ujerumani pia siku ya 23 Julai 2016 katika tamasha kubwa la International Afrika Festival Tubingen,
siku ya 30 Julai 2016 watatumbuiza XXL Afro Sommer Jam mjini Stuttgart katika Kutur Arena. mzimu huo wa muziki wa bongo dansi utaendelea kudatisha washabiki siku 13 Agosti 2016 mjini Frankfurt katika Afro-Karibik    viwanja vya Robestock Park,Frankfurt,Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya imefanikiwa kuwanasa maelfu washabiki kwa wingi inayoongozwa na mwanamuziki nguli  Ebrahim Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika maonyesho hayo makubwa na ya aina yake kwa mashabiki wa muziki katika maonyesho hayo, ambapo  watakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.

Bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Mapenzi ya Pesa" na single CD ya "La Mgambo" pia msikose kusikiliza nyimbo "Supu ya Mawe" ,''Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo zipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" zote zinasikika katika kambi ya FFU au web yao


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments