[wanabidii] UJUMBE WA VIJANA WALIOSHIRIKI MATEMBEZI YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

Friday, January 10, 2014

UJUMBE WA VIJANA WALIOSHIRIKI MATEMBEZI YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI.

 

UTANGULIZI.

 

Vijana wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama Cha mapinduzi (UVCCM) walioshiriki matembezi ya kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi yaliyofanyika katika wilaya zote za mikoa yote ya Zanzibar. Matembezi hayo yalianza mnamo tarehe 22nd Dec 2013, wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (ZNZ) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Dr Ali Mohamed Shein na kuhitimishwa tarehe 05th January 2014 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Taifa) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, katika viwanja vya Maisara, mkoa wa Mjini Zanzibar.

 

UJUMBE.

 

Kwanza kabisa tunashukuru Mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kusafiri salama, kushiriki matembezi kwa takriban wiki mbili kwa Amani na hatimaye kurudi tukiwa ni wazima wenye Afya tele, na kwamba hakuna hata mmoja wetu ambae amepata matatizo ya aina yeyote kwa siku zote ambazo tumeshiriki matembezi hayo muhimu.

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa hilo.

Pili, Vijana tunatoa pongezi za shukrani kwa uongozi wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) hasa kwa upande wa Zanzibar kwa mapokezi mazuri, upendo waliotuonyesha, ushirikiano wao na huduma ambazo tumekuwa tumepatiwa katika siku zote ambazo tumeshiriki matembezi hayo. Tunasema Ahsante sana na tunawaombea kwa Mwenyezi mungu azidi kuwaongezea neema na kuwafanya Viongozi bora zaidi kwa watu wake.

Baada ya shukrani na pongezi, ujumbe wa vijana unakusudia kueleza kwa mukhtasari maudhui ya ushiriki wao na manufaa yake ikiwa ni pamoja na mafunzo na ufahamu tulioupata kwa kushiriki matembezi hayo ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi.

·         Tunaunga mkono, kupongeza na kuenzi Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964. Kwani Mapinduzi hayo ni alama ya ukombozi wa wanyonge waliokandamizwa, kuonewa na kudhulumiwa haki na utu wao. Hivyo kama ilivyokuwa kwa ASP Youth League sisi Vijana wa UVCCM tunaunga mkono na kuenzi juhudi hizo zilizofanyika za kujenga jamii yenye usawa na isiyo na ubaguzi, tunaahidi kuendelea kuyaenzi, kuyaheshimu na kuyalinda Mapinduzi na wanamapinduzi.

 

Tuliamua kwa dhati ya mioyo yetu kushiriki matembezi hayo ya amani kwa lengo la kutoa ujumbe na kuonyesha hisia zetu kwa watanzania na dunia kwa ujumla, tukikumbuka na kuyataja majina ya viongozi wetu waliojitolea kupigania ukombozi, kuondoa dhulma, unyonge na unyonyaji wa kikoloni na kupata Taifa huru lenye kutoa haki kwa Raia wake.

 

·         Aidha, kwa kutambua kuwa Mapinduzi ya mwaka 1964 ndio chachu ya muungano, vijana tunasema kuwa tutahakikisha kuwa tunalinda na kutetea muungano na tunu zake. Tunatambua kuwa ipo mitazamo inayolenga kudhohofisha dhana mzima ya Muungano na kwamba ziko juhudi za kuvunja na kutugawa kama Taifa. Vijana tunatambua haki na wajibu wa kutetea Utu na Umoja.

UVCCM tutakuwa mstari wa mbele kuona kuwa Muungano unaendelea kuimarika na hatuoni aya kusema hadharani na kutofautiana na mtazamo wa tume ya mabadiliko ya katiba kuwa tunaamini katika  muungano wa serikali mbili na kwamba ndio mfumo bora ambao utaendeleza na kuimarisha Muungano. Lakini pamoja na kutofautiana na tume juu ya muundo wa muungano bado tunaipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka sasa.

 

Imetolewa na:

 

Sylvester Yeredi

Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa (UVCCM)

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments