[wanabidii] Mheshimiwa Harrison Mwakyembe mwanasheria anayebaka sheria kusudi

Monday, January 27, 2014
Itakumbwa kwamba mnamo tarehe 23 Agosti 2012, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi alimteua Madeni Juma Kipande kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimiamizi wa Bandari Tanzania,(TPA).--Uteuzi huu ulifanyika baada ya Mwakyembe kutoa tuhuma zisizothibitishwa--kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati huo, Ephraim Mgawe alishindwa kuiongoza TPA kwa uadilifu.- Hakuishia hapo, Mwakyembe alivunja Bodi ya Wakurugenzi na kuteua Kamati ya Uchunguzi ambayo -alisema -ingelifanya kazi kwa muda wa wiki mbili, na kuahidi kuwa muda huo ungelitosha kuthibitisha tuhuma zake -dhidi ya Mgawe na manaibu wake ili hatua za kisheria zichukuliwe.- Miongoni mwa tuhuma zilizoelekezwa kwa Mgawe lilikuwepo suala la kutoa ajira kwa upendeleo na kuajiri ndugu, jamaa, marafiki na kadhalika pasipo kufuata taratibu na kanuni za ajira kwenye mashirika ya umma.- Tuhuma nyingine zilihusu kushindwa kusimamia miradi na hivyo kulisababishia taifa hasara.
-
Uvunjaii wa Sheria:Kutokana na tuhuma hizi na nyinginezo dhidi ya Mgawe na wenzake, Mwakyembe aliiamrisha Bodi ya Wakurugenzi wa TPA kuwasimamisha kazi maafisa mbali mbali wa TPA ili kupisha uchunguzi.- Bodi hii ilikuwa chini ya unyekiti wa Raphael Mollel, na ilisheheni wajumbe wenye weledi na wazoefu katika nyanja zao mbali mbali. -Bodi ya wakurugenzi -chini ya Mzee Raphael Mollel ilimuomba Mwakyembe aweke kwa maandishi agizo lake hilo la kuwasimamisha viongozi hao wakuu wa TPA .---Waziri ilibidi kwa shingo upande akubaliane na Bodi na kuweka agizo lake--kwa maandishi kupitia barua iliyotiwa saini na Mwakyembe mwenyewe, huku akitambua -fika kwamba amri na barua kama hiyo, kama kungekuwepo na ulazima au sababu, basi ilibidi barua hiyo itiwe saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, lakini yeye aliamua kuvunja sheria na utaratibu halali wa kiutawala kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa vile udharura wa yeye kuvunja sheria haukuwepo kabisa.- Hii imepelekea Mwakyembe kushitaliwa mahakamani yeye binafsi na mmoja wa maafisa hawa walioachishwa kazi.
-
Wiki mbili ziliisha na Mwakyembe bila aibu wala soni, alikuwa akiongeza muda wa Kamati ya Uchunguzi wiki baada ya nyingine. -Hatimaye -ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ilikabidhiwa -mwezi wa Desemba 2012.- Baadaye, wananchi walitangaziwa hatua ya kuwaachisha kazi Mgawe na maafisa wengine, na kama kawaida yake, Mwakyembe aliahidi kuwa kazi zote zitatangazwa ili zishindaniwe na Watanzania wote ili kupata watu wenye uwezo kushika nafasi hizo na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.- Kumbe ahadi hii ilikuwa ni danganya toto tu, Mwakyembe aliendelea kuvunja sheria kwa kumlinda Kipande ili aendelee kukaimu nafasi hiyo, na ajira hizo hazikutangazwa hadi mwezi wa Mei 2013, bila shaka baada ya Mwakyembe kupata shinikizo la kufanya hivyo.
-
Juhudi za kumsimika Kipande kinyemela zilipofanikiwa, Mwakyembe ikawa sasa kachonga mzinga na hivyo akaendelea kulamba asali.- Kati ya Agosti 2012 na Januari 2014, Mwakyembe akiwa kama mwanasheria aliyebobea, amefanya uvunjaji wa sheria tena kwa makusudi, ili kulinda maslahi yake binafsi kwa kiasi kikubwa sana, hasa ikizingatiwa kuwa mambo mengi anayafanya kwa usiri mkubwa kwa kumtumia Kipande, Bodi ya TPA na baadhi ya viongozi wa wafanyakazi wa TPA.- Uvunjaji huu wa sheria, kanuni, taratibu na haki za binadamu umejikita katika maeneo na matukio mengi ikiwemo:
-
(i)------------ Amri ya kuwasimamisha kazi maafisa wa TPA kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa kutoa barua ambayo alitia saini yeye mwenyewe Mwakyembe mwezi Agosti 2012 badala ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambavyo ni kinyume cha sheria ya kazi za umma, utawala bora na kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali.
(ii)---------- Uteuzi wa kiini macho wa Madeni Kipande kwa wiki mbili, na kuishia kumkingia kifua hadi leo hii, kwa kuingilia kati, sio tu mchakato wa usaili, bali hata kuivunja bodi ya wakurugenzi, katika kipindi cha mwaka mmoja, aliyoichagua kwa mbwembwe na bashasha zote.- Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, baada ya kugundua janja ya Mwakyembe kuwatumia kwa faida yake, wakati wao wakijidhalilisha kwa kuvunja uadilifu wao, waliamua kumwadabisha Kipande kutokana na ukosefu wa nidhamu,n a pia uwezo wake mdogo kiutawala uliosabababisha Kipande kushindwa -kuiongoza taasisi kubwa kama TPA.
(iii)--------- Kuvunja sheria mama ya TPA (Port Act of 2004) kwa kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini bandari ya Mtwara kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPA. Sheria mama hii inatamka wazi kuwa mtu yeyote mwenye maslahi yanayokinzana katika Mamlaka ya TPA asiwe mjumbe wa bodi.- Uteuzi huu umefanyika kwa makusudi, ili mjumbe huyo alinde maslahi ya Mwakyembe kwa nguvu zote, ili na yeye ajihakikishie maslahi yake binafsi kutokana na marupurupu na posho nono za bodi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mteule huyo alikimbia umande na hajawahi kukanyaga darasani.
(iv)--------- Uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi TPA kwa urafiki badala ya utaalamu, weledi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, hususan sekta ya bandari ili kusimamia kwa umadhubuti taasisi hii muhimu ambayo kwayo nchi hii inaweza kuvuka kutoka kwenye dimbwi la umaskini.
(v)---------- Kushurutisha ajira za upendeleo kwa ndugu, jamaa, rafiki, familia na ukoo wa Mwakyembe na wenzi wao kadri atakavyo.- Mwakyembe kati ya Agosti 2012 na Januari 2014 ameshinikiza ajira za upendeleo bila kwa mtoto wa dada yake na ndugu zake wengine, ajira za watoto wa vigogo mbalimbali, ajira ya "Mkurugenzi wa Inteligensia" ambayo wala kwenye ikama ya TPA haipo kabisa, na baadae kushinikiza bodi kumwajiri mtu huyo kama Meneja Mipango, wakati hana taaluma yoyote katika maeneo haya.
(vi)--------- Kubuni miradi lukuki kwa maslahi yake binafsi kama ule wa nyumba ya wageni utakaogharimu zaidi ya shilingi 500.0 milioni jimboni kwake Kyela, Matema Beach. Miradi mingine ni kama ule wa kituo cha makasha cha SUKITA kwa kisinginzio cha kutunisha mfuko wa chama tawala, kumbe ni kwa faida yake binafsi na wapambe wake kama Kipande.
(vii)------- Kutoa amri ya kuvunja sheria ya manunuzi -kwa kuilazimisha bodi ya wakurugenzi TPA kutoa maamuzi ya kuiamuru menejimenti ya TPA aidha kuingia ubia na makampuni au watu binafsi bila kutangaza zabuni kama sheria ya manunuzi inavyoainisha, ili kuhakikisha kuwa maslahi yake binafsi yanazingatiwa na yanalindwa na kampuni hizo au na watu hao.- Mradi wa kujenga visima vya mafuta (storage tanks) ambao amedhamiria kuutoa pasipo tenda yoyote kwa kampuni moja ya kiitaliano. Miradi miwili kapania kuitoa kwa kampuni za kibelgiji bila tenda ambayo ni -mfumo wa ukusanyaji taarifa za mizigo (ECTN) ambao wadau waliukataa kwa vile ni wa kiutapeli na hauna faida kwa Taifa.- Kwa kuzingatia sababu hizi mahsusi, SUMATRA waliupiga chini mradi huu wa ECTN, lakini Mwakyembe mnamo mwezi wa Desemba mwaka jana, ameshurutisha Bodi na menejimenti kuutekeleza mradi huu, ambao utamwezesha Mwakyembe na washirika wake kutengeneza faida ya zaidi ya dola za kimarekani milioni mia moja kwa mwaka, kwa kazi hewa.- Mradi mwingine kwa kampuni ya kibelgiji ni wa ujenzi wa gati mbili za makasha hapo Gerezani creek, badala ya kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa gati 13 & 14 na wachina.
(viii)------ Kushinikiza ununuzi wa ardhi ya kigogo mwenzake Kisarawe kwa ajili ya mradi wa bandari kavu. -Mwakyembe aliiagiza bodi kuwa TPA iingie kwenye mkataba na kigogo mmoja kutoka Zanzibar (jina tunalo) kwa lengo la kukodisha au kununua eneo/ardhi ya kigogo huyo Kisarawe kwa zaidi ya shilingi 16 bilioni au kuendeleza eneo hilo na kigogo huyo ili kumwezesha Mwakyembe na wenzake kupata mrahaba pasipo jasho. Mwakyembe alitoa agizo hili bila kuzingatia ukweli kuwa Wizara ya Ardhi tayari ilikuwa imeridhia TPA kupatiwa ardhi na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya mradi huu ulioko chini ya Big Result Now. -Wananchi wa Kisarawe wangelipwa fidia na TPA kama sheria inavyoelekeza.- Mwakyembe aliingilia mchakato huu mwezi wa Desemba mwaka jana huko Mtwara, na kuamrisha mazungumzo kati ya Mamlaka na kigogo huyo kuanza mara moja, chini ya usimamizi wa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu na Idara ya Mipango TPA.
(ix)--------- Kutangaza jina baya la wizi kwa bandari ya DSM kuwa makontena yapapotea kama kiberiti bandarini bila kutilia maanani athari za tamko hili kwa mamlaka.
(x)---------- Kutangaza ongezeko hewa la mapato ya TPA kwa wananchi kwenye vyombo vya habari -kuwa mapato yamefikia wastani wa shilingi 50.0 bilioni kwa mwezi, kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa na mamlaka hiyo.
(xi)--------- Kuwapakazia wajumbe wa bodi aliyoivunja kuwa aliwafukuza kwa ajili ya kuigeuza TPA shamba la bibi kwa kulazimisha safari za nje ya nchi kila mara na mikutano ya bodi nje ya ratiba, huku Mwakyembe akifahamu kuwa hii ilikuwa njama yake ya kupindisha ukweli. Inafahamika wazi kuwa safari hizi za ng'ambo na vikao vya bodi nje ya ratiba mara kwa mara, kama ilivyo ada hata leo, Mwakyembe huvitumia kuwarubuni wajumbe wa bodi ili wawe baridi".- Kafanikiwa kwa bodi hii inayoendelea, -lakini alijaribu mbinu hizi kwa bodi iliyovunjwa bila mafanikio.
(xii)------- Kudanganya umma kuwa ugunduzi wa wizi wa mafuta kutoka bomba la mafuta kwa kutumia puto kubwa aliugundua yeye, kumbe si kweli.- Ukweli ni kwamba wizi huu uliripotiwa na wadau kwenye mahojiano na Kamati ya Uchunguzi aliyoiunda Mwakyembe, dhidi ya viongozi wa TPA mwaka juzi.- Lakini kwa mshangao mkubwa, mwezi wa Septemba mwaka jana, yaani baada ya mwaka mmoja, Mwakyembe aliibuka kama shujaa kwa kuitisha waandishi wa habari na kujigamba kuwa aliibua aina ya wizi huu mpya, kama vile kagundua lulu, kumbe ilikuwa ni uongo. -Ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ni ushahidi tosha.
(xiii)------ Kupuuza dhana ya utawala bora, ukweli na uwazi katika uendeshaji wa taasisi hii kubwa, kwa kuwa yeye Mwakyembe amekuwa kama mtendaji mkuu wa TPA kwa kusimamia kazi za kila siku na kufanya kama atakavyo.
(xiv)------ Kutumia rasilimali za TPA vibaya na kwa matashi yake pasipo kufuata sheria na kanuni za fedha za Serikali.- Kwa mfano, Mwakyembe anaamrisha baadhi ya matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kugharamiwa na TPA ikiwemo posho za vikao na safari, takrima, n.k- Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu imetoa mifano hai kwenya ripoti yake ya ukaguzi kuhusu dhahama hii.
(xv)--- Kutumia viongozi wa chama cha wafanyakazi wa TPA kumlinda Kipande kwa kuwapatia viongozi hao marupurupu yasiyo na kifani ili kuwarubuni wakae kimya dhidi ya dhuluma ya wafanyakazi wa TPA aliyoianzisha yeye Mwakyembe kwa tuhuma za kubambikizwa. Hii imesababisha TPA kupata kesi nyingi za ukiukwaji wa haki za binadamu na madai ya compensation.
(xvi)- - Kushinikiza uteuzi wa wafanyakazi wa ngazi za chini kushika nyadhifa za juu za uongozi, pasipo sababu maalumu, ila tu ya kujuana (know who) na sio ya uwezo wa mtu (know how). -Hii imesababisha manung'uniko makubwa miongoni mwa wafanyakazi TPA, ambao waathirika wanajiona kama watoto ya tima, na wale walionufaika kwa kukaimu nafasi hizo za juu, wanawatambia mabosi wao, kwa kusema kuwa kutesa kwa zamu. Wakati mwingine, meneja wa kitengo anawajibika kwa ofisa mwandamizi au hata ofisa tu mdogo, ambaye labda kateuliwa kushika nafasi ya ukurugenzi kwa uswahiba tu.
Wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi : Chonde chonde Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mheshimiwa Jaji Kiongozi, kwa heshima na taadhima, mnaombwa kwa pamoja mfungue macho yenu muone, na masikio msikie ili mfahamu kinagaubaga, migongano na migogoro ya mwanasheria Mwakyembe, aliyebobea katika sheria na kuzivunja kwa hila, ili mchukue hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuwa kadhalilisha taaluma ya sheria.- Haya sio makosa ya kisiasa, bali ni uvunjwaji wa sheria, uliukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa taaluma ya sheria ambayo nyie mnaisimia vizuri.
-
Kama alivyowahi kutamka kwa Waziri Mkuu Mstaafu mmojawapo, na yeye haina budi kupima huu uchafu wake na kujiondoa, au akikataa, basi aondolewe.- Huyu sio Waziri mzigo, bali ni Waziri hatari anaetumia mali ya umma kujitajirisha yeye na ukoo wake na hivyo kutudidimiza sisi walalahoi, tumemchoka.. Ikulu isiishie kumwambia tu uchunguzi huru ufanywe haraka. Kila taasisi zimechoka kuanzia TRA, polisi na wadau anavuruga bandari.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments